Mchezaji wa klabu ya Chelsea Michael Ballack anaamini kwmaba mabingwa wa England Manchester United, watadhoofika msimu ujao baada ya kuondoka kwa mchawi wao wa magoli na kutabiri kwmaba utakuwa ni msimu wa Chelsea.
Ujio wa kocha mpya Carlo Ancelotti katika dimba la Stamford Bridge kumefufua tumaini jipya la kwa mashabiki wa Chelsea na huenda ukawa msimu wa mafanikio ya ubingwa tangu mara ya mwisho wa twao mwaka 2006.
Kiungo mchezeshaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani anaamini watafanya vizuri zaidi ya Manchester United ambayo imempoteza Cristiano Ronaldo na Carlos Tevez katika dirisha la usajili.
Amesema lengo lao kila msimu huwa ni kutwaa ubingwa na wanaamini watatwa ubingwa msimu huu.
Amekiri kuwa msimu uliyopita walianza vema lakini Man United walicheza katika kiwango cha juu zaidi yao.
Na kukiri kwamba mashetani hao wekundu wa Old Traford wamekuwa kikwazo kikubwa kutwaa ubingwa msimu wa 2007 na 2008.
No comments :
Post a Comment