Wachezaji wa timu ya soka ya Simba wakiwa mazoezini Chukwani mjini Zanzibar kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Haya ni maandalizi ya klabu ya Simba iliyojichimbia visiwani Zanzibar kabla ya ligi kuu Tanzania bara!
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Simba, Patrick Phiri amesisitiza msimamo wake kwamba timu yake inatisha mwaka huu, na kuna uwezekano wa timu hiyo kuweza kutwaa ubingwa wa hata kabla ya ya ligi kumalizika.
Kocha huyo raia wa Zambia amesema kutokana na maandalizi yanavyokwenda, watani wao wa jadi Yanga, ambao msimu uliopita waliwatambia kwa kuwafunga mara moja na kutoka nao sare mara moja, safari hii watarajie kipigo kutoka kwa timu yake.
Kocha huyo aliyekuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi Chukwani mjini hapa ambapo timu hiyo imeweka kambi, ameusifu uongozi wa Simba ulivyojipanga vizuri katika maandilizi na hivyo kurahisisha ratiba yake ya mazoezi.
Phiri alifahamisha kuwa, tangu timu ilipowasili hapa Jula 19, hakuna tatizo lililojitokeza kwa vile pahala walipofikia pameandaliwa vizuri ambapo wachezaji na
uongozi uliopo hapa wamepafurahia.
"Maandalizi ni mazuri, hakuna malalamiko kutoka kwangu wala kwa wachezaji, sana sana
uongozi umenipa deni kubwa la kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Bara mwaka huu, "
alisema Phiri.
Alisema, anajua jinsi mashabiki wa Simba walivyokuwa na kiu ya kuiona timu yao inatwaa ubingwa, nawaahidi kiu hiyo itamalizika na ubingwa huo utapatikana tena kwa kuwafunga watani wetu wa jadi," alisema.
Alisema, Simba ilikuwa nzuri tangu msimu uliopita lakini ilifanya vibaya, kutokana na kukosa stamina pamoja na ufundi, lakini msimu huu inatisha kwa sababu kamati ya usajili imefanya kazi nzuri.
"Hadi hivi sasa siwezi kusema mchezaji gani yupo mbele zaidi kwa mazoezi, wote wanajituma sana, na kama utawachunguza vizuri huwezi kumjua yupi mgeni na yupi mwenyeji kwa kweli wananipa raha sana," alisema.
No comments :
Post a Comment