TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajia kujipima nguvu na moja kati ya timu zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya pili ya kuwania kufuvu kucheza Kombe la Dunia 2010 na Kombe la Mataifa Afrika.
Mchezo huo ambao Stars itakuwa ugenini umepangwa kufanyika katika tarehe inayotambuliwa na FIFA ambayo ni Agosti 12.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbrazil Marcio Maximo alisema wameomba kucheza na moja kati ya timu hizo ambazo ni ngumu ili kujipima uwezo wao.
Alisema mchezo huo utakuwa ni kipimo kizuri kwao katika kujenga kikosi hicho ndio maana wameomba kucheza na timu yenye uwezo mkubwa Afrika.
"Tumeomba kucheza kati ya timu hizo zilizofuvu hatua ya pili na mategemeo yetu tutapata timu mojawapo kwani tumeomba zaidi ya timu tano ambazo zipo juu kiuwezo katika hizo zilizofuvu," alisema Maximo.
Alisema mategemeo makubwa kupata timu bora zaidi katika timu hizo 20 ambazo zimefuvu bila kuangalia kama kuna baadhi tayari waliwahi kucheza nazo.
Maximo alisema anatarajia kutangaza kikosi hicho Julai 30 huku kukiwa na wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje ya nchi pamoja na wachezaji wa ndani.
Alisema kikosi hicho kinatarajia kuanza kambi Agosti 3 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania katika chati ya FIFA.
Nchi za Afrika ambazo zimeingia katika hatua ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza kombe la Dunia na michuano ya Afrika ni Gaboni, Togo, Moroko, Kameruni, Tunisia, Nijeria, Kenya
Msumbiji, Aljeria, Misri, Zambia, Rwanda, Ghana, Mali, Benin, Sudan, Kodivaa, Burkina Faso, Guinea na Malawi.
Katika chati ya viwango vay FIFA, Tanzania kwa sasa ipo katika nafasi ya 97 baada ya kuifunga mabingwa wa Oceanic, New Zealand mabao 2-1 katika mchezo uliocheza mapema Juni.
Na Erasto Stanslaus
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment