Mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Kigoma, Katunka Amani (kulia) na Isihaka Athumani wa Morogoro wakiwania mpira wakati wa mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Morogoro ilishinda bao 1-0.
TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya ya Mkoa wa Morogoro imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya vijana yanayoelekea ukingoni baada ya kuichapa Kigoma mabao 1-0.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru na kushuhudiwa na umati wa mashabiki wa mpira wa miguu, walishuhudia Kigoma wakikosa mabao mengi dakika za mwanzo.
Morogoro ambao walitolewa na Tabora katika mechi ya nusu fainali, walijiaptia bao pekee dakika ya 20, lililofungwa na Hamis Salehe kwa mpira wa kona uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Baada ya kufungwa bao hilo, Kigoma walijaribu kufanya mashambulizi langoni mwa Morogoro, lakini washambuliaji wake, Baruan Akilimali na Matata Seif walishindwa kukwamisha mpira wavuni dakika za 70 na 78.
Kutokana na ushindi huo, Morogoro walizawadiwa fedha sh. milioni mbili kutoka kwa waandaji wa mashindano hayo ya vijana.
Jumamosi, timu ya Mjini Mgharibi ambao walionesha soka safi katika mechi zao za nyuma, wataumana na Tabora katika mchezo wa fainali utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment