SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limezitaka klabu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kuweka wazi viwanja watakavyotumia na kuwasilisha rangi za jezi watakazotumia kwa michezo ya nyumbani na ugenini.
Msimu uliopita kulikuwa na mabadiliko kwa baadhi ya viwanja ambapo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kulikuwa na timu za Yanga, Simba, Moro United, JKT Ruvu ya Pwani na Azam FC zote ziliutumia uwanja huo.
Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Fredrick Mwakalebela alisema, walizitumia klabu zote za ligi kuu, taarifa ya kuzitaka ziweke wazi viwanja watakavyotumia kwa ajili ya msimu ujao, pamoja na kuwasilisha rangi za jezi watakazozitumia.
''Unajua muda uliobaki ni mchache kabla ya ligi kuanza, hivyo jana (juzi) tuliziandikia klabu mambo mbalimbali yakufanya kabla ya ligi kuanza, lazima watuambie mapema watatumia jezi za rangi gani watakapokuwa ugenini na nyumbani pamoja na viwanja watavyotumia,'' alisema Mwakabela.
Alisema ni lazima vitu hivyo vipelekwe mapema, ili na wao wapate muda wa kupanga ratiba ya ligi hiyo, kwani klabu zikishindwa kutoa taarifa mapema, watashindwa kupanga ratiba kwa kuwa hawatajua ni viwanja vingapi vitatumika kwa ligi hiyo.
Mwakalebela alisema mbali na hayo, pia wamezitaka klabu hizo kuwasilisha logo (nembo) za wadhamini wao, ili wajue ni jinsi gani watakavyowaelekeza mahali zitakapokaa kwenye jezi ukizingatia kuwa, ni lazima nembo ya mdhamini mkuu ambayo ni Kampuni Vodacom iwe mbele.
Akizungumzia suala la kiungo wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' na Simba, Henry Joseph kama Shirikisho la Mpira wa Miguu la Norway limemwombea uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya kuichezea Kongsvister ya nchini humo, alisema mpaka sasa hawajapokea barua yoyote kutoka huko.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
1 week ago
No comments :
Post a Comment