Golikipa wa klabu ya Newcastle Steve harper amedai klabu hiyo inakufa taratibu, kifo cha maumivu huku mmiliki Mike Ashley akijaribu kuiuza klabu hiyo bila mafanikio.
Wanunuzi kadhaa wamekuwa wakitangaza nia yao ya kutaka kuinunua kabla ya kushuka daraja na baada ya kushuka daraja lakini wamekuwa hawafikii makubaliano na hatimaye kupotea kusiko julikana.
hatua hiyo imemuacha Alan Shearer njia panda asijue lini atasaini mkataba wa kuinoa timu hiyo, huku wachezaji nao wakiwa katika giza totoro lisilo hata lepe la mwanga la kuwaonyesha njia.
Harper akizungumza kwa uchungu amesema inauma sana inapofika wakati mtu unakuwa hujui nini cha kufanya, huku wachezaji nao wakijua bosi wao maji yamemfika shingoni, licha ya kuwa na ndoto za Alinacha kwamba siku moja watajenga nyumba angani na kuwa matawi ya juu.
Amesema kila moja, mashabiki, wachezaji, uongozi wanataka kuijenga upya klabu hiyo lakini hali ndiyo inazidi kuwa ngumu kila kukicha.
MIMEA VAMIZI NI TISHIO KWA IKOLOJIA YA HIFADHI ZETU, BALOZI POLEPOLE
-
Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humprey Polepole amesema uwepo wa mimea
vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa inaathiri na kubadilisha ikolojia ya
mae...
1 day ago
No comments :
Post a Comment