|
Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga kulia akizungumza
na waandishi wa habari juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano la
Taifa la Redds Miss Tz kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz
Bosco majaliwa |
Fainali za
shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika
ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini D’salaam
Akizungumza na waanmdishi
wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim
Lundenga alisema maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari na leo
tupo hapa kuwatangazia watanzania na washika dau wote wa tasnia ya Urembo kuwa
tiketi kwaajili ya shindano letu la mwaka huu zipo tayari na zipo kwa idadi
maalum na leo hii zinaanza kuuzwa katika vituo tulivyovipendekeza kulingana na
maoni ya wadau
Kutokana na
ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini
watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila
tiketi itagarimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za kitanzania.
Katika
kufanikisha shindano hili kutakuwa na vitu tofauti na miaka ya nyuma na
tutarajie kuona shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu
kubwa ya warembo wetu ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini
Vituo vinavyoanza
kuuza tiketi hii leo ni. Stears samora
Regency park
Hotel,Rose garden Mikocheni,Share illusion-Mlimani City,Giraffe Hotel,Ubungo
Plaza na ofisi za Lino.
Nitoe rai kwa
wapenzi wote waweze kupata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu ya
kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali
Kwa upande wa
burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa
nchini kama
1) Diamond Platnum
2) Winfrida Josephat’Rachel’
3) Wanne star ngoma troupe
Katika shindano
hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo yanayojulikana kama [Fast
Tract] Tayari washiriki 5 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika kundi la
Warembo 15 Bora. [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni
Lucy Stephano –
Miss Photogenic
Magdalena Roy –
Top Model
Mary Chizi – Top
Sport Woman
Babylove Kalalaa
– Miss Talent
City sports
lounge-iliyopo posta mpya mkabala na mnara wa askari.
Happiness Daniel
– Miss Personality
Mwisho napenda
kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha
Redds Original,Star Tv na Giraffe Hotel
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI