WAKALI 12 WA 'THE MIC KING' WAPATIKANA KUTOKA KINONDONI
Washiriki wa shindano la The Mic King, waliofuzu kuingia 12 bora kutoka Kinondoni wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Kundi la Wakali Dancers likiwajibika stejini.
USIKU
wa kuamkia leo kulifanyika mchujo mkali wa kuwasaka wakali 12 kutoka
Kinondoni wa shindano la The Mic King, ndani ya Ukumbi wa burudani wa
Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam. Baada ya kumenyana vikali kwenye
steji hiyo huku wakifuatiliwa kwa makini na majaji wanaoujua muziki
vilivyo John Dilinga (Dj JD), na Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, ambao
walifanya upembuzi makini na kuwapata wakali hao ambao ni Martin Gasper,
Jafaar Kassim, Lusajo Kapngala, Peter Lugaman, Emmanuel Clemence, Ally
Zuberi, Abdi Salim, Omary Xavery, Modestus Luiza, Athuman Ayoub,
Dickson Siwalaza na Hudu Juma.
Shindano hilo pia lilisindikizwa na burudani za muziki kutoka kundi la Wakali Dancers na bendi ya Taarab ya Mashauzi Classic.
Majaji wa mchakato huo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (kushoto) na John Dilinga (Dj JD) wakiwa kazini.
Isha Mashauzi akiwarusha roho mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Dar Live.
Mpiga kinanda maarufu Bongo, Thabit Abdul akitumbuiza jukwaani.
No comments :
Post a Comment