Mwezeshaji
wa Jukwaa kutoka Tigo Makao makuu Hubert Luis akifungua Jukwaa hilo
ndani ya Hoteli ya Gold Crest Mwanza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Tigo
Diego Gutirrez.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leoimezindua majukwaa kwa ajili ya
wajasiliamali wapya nchi nzima kama sehemu ya wajibu wake katika
kusaidia na kukuza wajasiliamali wadogowadogo na wakati nchini.
Lengo la majukwaa hayo ni kuwaleta pamoja wajasiliamali na mashirika ya
kibiashara kutoka sekta mbalimbali ili kupanua mitandao yao na kunufaika
na suluhu mpya za mawasiliano kwa biashara. Biashara ndogo na za kati
zitanufaika na warsha, mafunzo na mazungumzo ya mada zinazohusu masoko,
menejimenti, fedha na uzalishaji.
|
No comments :
Post a Comment