Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, October 30, 2012

MAZOEZI YA SIMBA KWA AJILI YA MCHEZO DHIDI YA POLISI MORO SC LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA JAMHURI MOROGORO 0KTOBA 31/ 2012..


 EMMANUEL OKWE KUSHOTO AKIPIMANA UBAVU NA FELIX ZUNZU WAKATI WA MAZOEZI YA KLABU YA SIMBA KWA AJILI YA MCHEZO BAINA YA TIMU HIYO NA POLISI MORO SC KATIKA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA JIONI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.
 DANIEL AKUFF (KATIKATI) AKIWA AMENYANYUA DALUGA WAKATI AKIWANIA MPIRA DHIDI YA AMRI KIHEMBA KULIA HUKU HARUNA SHAMTE AKIUPIGIA MAHESABU MPIRA HUO.
 UHURU SELEMAN (16) AKITAFUTA NAMNA YA KUWATOKA WACHEZAJI WENZAKE MWINYI KAZIMOTO.
 WACHEZAJI WAKIOMBA DUA MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MAZOEZI.
MASHABIKI WA KLABU YA SIMBA WAKINGALIA MAZOEZI YA KLABU HIYO.
MENEJA wa klabu ya Polisi Moro Sport Club na Msemaji wa klabu hiyo, Clement Bazo amesema kuwa klabu yake itaibuka na ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara klabu ya Simba katika mchezo wao wa ligi hiyo utaopigwa kesho kwenye uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:30 mkoani hapa.
Bazo alisema kuwa mchezo huo utakuwa mchezo wao wa tisa tangu kuanza kwa ligi hiyo na kupoteza michezo sana na kutoa sare mbili na kujikusanyia pointi mbili wanauchukua mchezo huo kama michezo mingine baada ya kufanya vibaya hivyo lengo kuu ni kufanya vizuri na kuwa wamejindaa kukabiliana na vinara hao.
“Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa michezo iliyobakia hivyo kesho (leo) tunacheza na Simba hivyo sisi Polisi lengo letu tulilonalo kwa sasa ni kufanya vizuri ukiwemo mchezo wetu dhidi ya dhidi ya Simba SC na tunaasilimia 75 ya ushindi kwa mchezo huo”. Alisema Bazo.
Bazo alisema kuwa mchezo ni mchezo matokeo ambayo yanahitajika katika mchezo huo kama watashindwa kuwafunga Simba basi mchezo utaweza kumalizika kwa sare ya aina yo yote ile.
Naye Kocha Mkuu wa klabu ya Polisi Sport Club, John Simkoko amesema maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Simba yamekabili na anachosubiri ni dakika 90 kuweza kuamua matokeo ya mchezo huo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam ambako wameweka kambi katika jeshi la polisi Kulasini, Simkoko alisema kuwa wachezaji wake wote wapo fiti kwa mchezo huo na anachosubiri ni kuanza kwa mchezo huo dhidi ya vinara wa ligi ligi Simba Sport Club hii kesho.
Simkoko alisema kuwa waliweka kambi mapema katika jiji hilo baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu JKT kwa lengo kumalizia michezo iliyobakia ukiwemo na Simba katika uwanja wake wa nyumbani na kuwa dakika 90 ndizo zitakazoamua mshindi katika mchezo wa soka.
“Mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili na tumejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuikabili Simba hivyo najua Simba wanahitaji ushindi nasi vile vile tunahitaji ushindi katika mchezo huo lakini dakika 90 ndizo siku zote zinaamua matokeo ya mchezo ikiwemo sare, kupoteza na ”. alisema Simkoko.
Katika mchezo huo utanarajia kuibua hisia nyingine kutoka kwa mashabiki Manispaa ya Morogoro endapo klabu hiyo ya Polisi Moro kama itaendelea kupoteza mchezo huo baada ya kupoteza mwelekeo kufuatia kufungwa michezo saba na sare mbili huku ikiwa na pointi mbili.

No comments :

Post a Comment