Balozi wa India nchini Kocheril Bhagirath akibadilishana mawazo na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM cha Jijini Dar es salaam Profesa Godwin Mjema na viongozi wengine wa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa shahada ya uzamili katika Biashara za Kimataifa – MBA-IB jana jijini Dar es salaam. Balozi Bharagath amesifu ushirikiano wa IFM na chuo kikuu cha Biashara cha India – IIFT katika utoaji wa kozi hiyo na hivyo kupunguza umuhimu wa watanzania kusafiri India kwa ajili ya masomo hayo.
Balozi wa India nchini Kocheril Bhagirath (katikati mstari wa mbele mwenye suti ya kijivu) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM cha jijini Dra es salaam Mkuu wa Chuo cha IFM akiwemo Profesa Godwin Mjema(kulia kwa Balozi) na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa shahada ya uzamili ya Biashara za Kimataifa – MBA-IB inayotolewa kwa ushirikiano wa IFM na Chuo Kikuu cha Biashara cha India – IIFT. Balozi Bharagath amesifu ushirikiano wa IFM na IIFT katika utoaji wa kozi hiyo hatua inayoimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili hizo na pia kupunguza umuhimu wa watanzania kusafiri India kwa ajili ya masomo hayo.
No comments :
Post a Comment