Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo hii imekabidhi vitabu20000 vya wiki ya nenda kwa usalama barabarani vilivyochapishwa kwa gharama ya shillingi million 36. Vitabu hivi vitagawiwa watumiaji wa barabara nchi nzima watumie kama njia mojawapo ya kurejea na kujikumbushia kuhusu utumiaji na usalama barabarani. Wiki ya usalama barabarani imeadhimishwa tangu, tarehe tatu 3 hadi tarehe 8 mwezi wa kumi mwaka huu.
SBL kama kampuni ya vilevi, tunatambua na tumekuwa mstari wa mbele kabisa katika kupigania unywaji wa pombe kwa ustaarabu . Tumekuwa tukikumbusha katika matangazo yetu yote kupitia bidhaa zetu kwamba unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kudhuru afya ya mnywaji.
Hivi karibuni tulizindua kampeni ya ‘Responsible Drinking’ yaani KUNYWA KWA USTARAABU’ ambapo Kampeni hii inalenga kuwakumbusha wateja wetu kwamba wasinywe pombe na kuendesha gari, ila wawe na dereva maalum ambaye hatumii pombe ndiye aendeshe au watumie usafiri mwingine wa kukodi.
Wiki ya usalama barabarani inalenga kuwakumbusha watumiaji wa barabara kuhusu sheria na kanuni za utumiaji wa barabara ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika ambazo zinasababisha vifo vya watanzania wengi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Usalama barabarani unahitaji jitihada kutoka kwa kila mtu’ ambayo imeadhimishwa rasmi kitaifa katiika mkoa wa Kagera.
No comments :
Post a Comment