Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) inapenda kuwafahamisha wananchi na wateja wake kwa ujumla kuwa kwa sasa kuna kazi ya uhamishaji wa njia za mawasiliano kandokando ya barabara mpya ya Bagamoyo ( Mwenge – Tegeta).
Kazi ya kuhamisha njia za mawasiliano ni inafanywa na wakala wa barabara (TANROADS) aliyeingia mkataba namba QTN/AE001/2009/2010/DSM/E/146 na mkandarasi.
Katika mkataba huu, Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) jukumu lake kubwa ni kuelekeza na kushauri njia mpya ya mtandao wa simu utakapopita tofauti na njia za awali.
Tunaomba ieleweke kuwa hadi hapo njia mpya ya simu itakapokamilika ndipo ile ya zamani itaondolewa kuepusha wateja kukosa huduma.
Tayari wakala wa barabara(TANROADS ) amekwishakamilisha awamu ya kwanza ya kuhamisha njia za simu kutoka Mwenge mpaka njia panda ya Africana. Na sasa kazi inaendelea kuanzia njia panda Africana kuelekea Tegeta.
Kwa vile kazi inahusisha njia za mawasiliano zilizopo juu na za chini ya ardhi, kitaalam kazi hii lazima iende sambamba na ujenzi wa barabara mpya kwa kuwa katika ujenzi , mkandarasi wa barabara anajenga njia za kupitisha mawasiliano baada ya kupima kina cha kwenda chini, kwani kina cha barabara kinafahamika tu pale udongo unapokuwa umechimbuliwa na mkandarasi wa barabara.
No comments :
Post a Comment