Sam Alardyce ameteuliwa kuwa meneja wa West Ham baada ya timu hiyo kushuka daraja.
Kocha huyo wa zamani wa Blackburn, Newcastle na Bolton anachukua nafasi ya Avram Grant, ambaye alifukuzwa kazi baada ya West Ham kushuka daraja huku ukiwa umebaki mchezo mmoja katika ligi kuu ya England.
"Ni klabu nzuri na yenye utamaduni mzuri na mashabiki thabiti," amesema Allardyce mwenye umri wa miaka 56.
"Nisingechukua kazi hii, kama nisingedhani tutarudi kucheza ligi kuu moja kwa moja."
Meneja wa muda wa West Ham Kevin Keen, ambaye alisimamia timu hiyo katika mchezo wa mwisho na kufungwa mabao 3-0 na Sunderland, alionesha nia ya kuiongoza klabu hiyo katika ligi daraja la kwanza.
Hata hivyo, Keen hana hana uzoefu wa kuongoza, mbali na kuishughulikia timu ya akiba ya West Ham.
Allardyce anataka kusajili wachezaji kadhaa katika juhudi za kutaka kupanda daraja katika msimu mmoja, na ameahidi kuwa na "mtazamo wa ushindi" kwa wachezaji.
No comments :
Post a Comment