Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, June 7, 2011

WAMA Kushirikiana Na FHI PAMOJA TUWALEE Kuwakomboa Yatima Wa Tanzania


|
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kushirikiana na mradi wa FHI PAMOJA TUWALEE wamedhamiria kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuwakomboa watoto yatima wa Tanzania.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete wakati akipokea taarifa ya kuutambulisha mradi wa FHI PAMOJA TUWALEE katika ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete alisema kuwa kwa kuwa malengo ya kazi ya taasisi zote mbili yanashahabiana ya kuwasaidia watoto yatima hivyo basi watafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa watoto hao wanasaidia na kuishi katika mazingira mazuri.
“Lengo kubwa la Taasisi zetu ni kuhakikisha kuwa mtoto yatima hanyanyaswi wala kubaguliwa na jamii inayomzunguka bali anaishi maisha mazuri, anapata elimu bora ambayo itamsaidia katika maisha yake”, alisema Mama Kikwete.
Akisoma taarifa ya mradi huo Priskila Gobba ambaye ni Mkurugenzi wa mradi alisema kuwa lengo kubwa walilo nalo ni kuboresha hali ya maisha ya watoto walio katika mazingira hatarishi na kaya zao kwa kuwajengea uwezo wana kaya na jamii ili watoe huduma kamilifu, bora na endelevu.
Gobba anasema, “Tumeamua kufanya kazi ya uhamasishaji na utetezi wa haki za watoto na WAMA kwani taasisi hii imekuwa ikiwasaidia watoto wenye mahitaji mbalimbali hapa nchini.”
Aliendelea kusema kuwa wamekuwa wakiwajengea uwezo watoto hasa wasichana ili wawe na ujasiri wa kujimudu kwa kuimarisha uwezo wao wa kuhimili athari za matukio mabaya yaliyowakuta, kujitunza, kujilinda na kujitosheleza kimaisha.
PAMOJA TUWALEE ni mradi ambao unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya Shirika lao la Maendeleo la hapa nchini (USAID Mission/Tanzania) na unafanya kazi zake katika wilaya 25 zilizoko kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Zanzibar. (Imeandikwa na Anna Nkinda wa MAELEZO)

No comments :

Post a Comment