Sepp Blatter amechaguliwa tena bila kupingwa kwa kipindi kingine cha miaka minne kuliongoza shirikisho la soka Duniani FIFA katika mkutano mkuu wa 61.
Blatter, ambaye sasa anaumri wa miaka 75 raia wa Uswis ambnaye amekuwa akiiongoza FIFA tangu mwaka 1998, amepata kura 186 kati ya 203 zilizopigwa.
"Kwa pamoja tutakuwa kwa kipindi cha miaka minne...kuendeleza mipnago yetu na kufanya kazi zetu," Blatter amewaambia wajumbe baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika na kutangazwa matokeo.
Mapema wajumbe wa mkutano huo walikataa mswada uliyowasilishwa na chama cha soka cha Uingereza wa kutaka kuahirisha uchaguzi.
Mpinzani wa Blatter, Mohamed bin Hammam alijitoea kuwania nafasi hiyo siku ya Jumapili baada ya kukabiliwa na tuhuma za rushwa.
Kiongozi huyo wa juu wa Shirikisho la kandanda Barani Asia, ambaye alifungiwa kuhudhuria mkutano huo, alitimuliwa sambamba na na wajumbe mwenzake Jack Warner, na FIFA imesema itafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo kupitia kamati ya maadili.
Msikilizaji na sasa tumfahamu Sepp Blatter.
* LIFE IN FIFA:
-- Baada ya Blatter kuahidi kwmaba hatosimama tena kugombea nafasi hiyo mwaka 2015, alikaririwa akisema baada ya uchaguzi huu hatokuwa tena hofu ya kuchaguliwa tena.
-- Blatter ameiongoza FIFA katika kuuza haki za matangazo katika Televesheni na wadhamini. Ana amesema shirikisho linazaidi ya bDola za marekani Dola bilioni moja katika akiba yake.
-- Blatter alijiunga na FIFA mwaka 1975 akiwa afisa maendeleo na amewahi kukaririwa akisema alijikuta akiwa na mapenzi na Afrika baada ya kutembelea Ethiopia mwaka 1976. Na aliweza kutimiza azma yake ya muda mrefu kwa kufanikisha fainali za kombe la Dunia kufanyika barani Afrika mwaka jana 2010 fainali zilizofanyika Afrika Kusini.
-- Alikuwa katibu mkuu wa FIFA mwaka 1981 na miaka 17 akiwa chini ya raisi wa FIFA kipindi hicho Joao Havelange, na kuchukua nafasi ya Uraisi toka kwa Mbrazili huyo mwaka 1998.
-- Blatter alikutana na mikingamo mingi mwaka 2002 wakati katibu mkuu wa FIFA kipindi hicho akiwa Michel Zen-Ruffinen kudai kuwa uchaguzi uliyomweka Blatter madarakani kuwa raisi wa FIFA mwaka 1998 ulitawaliwa na Rushwa.
-- mwaka 2004 Blatter aliwavutia wengi baada ya kupendekeza soka la wanawake wachezaji wake wavae bukta zinazobana.
-- alichaguliwa tena bila kupingwa mwaka 2007 kwa mara ya tatu.
* LIFE DETAILS:
-- Joseph S. (Sepp) Blatter alizaliwa mwezi March 10, 1936 nchini Swiss katika mji wa Visp.
-- alihitimu masomo yake katika shule ya Sion na St. Maurice colleges nchini Uswis na kisha kupata Shahada ya Biashara na Shahada ya Uchumi kutoka kitivo cha Sheria cha chuo kikuu cha Lausanne.
-- amekuwa akishiriki katika soka tangu mwaka 1948-1971, na anakumbukwa aliwa kucheza soka la ridhaa nchini Uswis katika ligi kuu. Alikuwa mjumbe wa bodi ya Xamax Neuchâtel FC kuanzia mwaka 1970-1975.
-- Blatter alianza safari yake kwa kuifanyia kazi taaluma yake aliyosomea akiwa Afisa Uhusiano katika kampuni ya Utalii ya Valaisan ya Uswis na mwaka 1964 alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Shirikiksho la mchezo wa Hockey la Swiss - Ice Hockey Federation.
No comments :
Post a Comment