
Timu ya Azam FC imeondoka Alhamisi Alfajiri ikiwa na wachezaji 22 na Viongozi 8 kuelekea Kagera kucheza mchezo wake wa kwanza na Kagera sukari katika uwanja wa Kaitaba mechi ambayo ni ya ufunguzi wa ligi kuu ya Tanzania Bara itakayoanza Agasti 23 mwaka huu.
Mwenyekiti Msaidizi wa Klabu ya Azam FC Said Mohammed amesema ligi kuu msimu huu itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zingine kupanda daraja na hata timu ambazo zimebaki zimezidi kujiimarisha zaidi.
No comments :
Post a Comment