Klabu ya Tunisia Etoile du Sahel imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya TP Mazembe ya Demokrasia ya Congo katika mchezo wa kundi B katika michuano ya ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mazembe ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli lakini mchezaji Ammar Jemal aliipatia goli la kusawazisha kwa mabingwa wa michuano hiyo ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2007 akiunganisha mpira wa adhabu uliyopipgwa na Sadat Bukari.
Mlinzi Aymen Abdennour alifunga goli la pili na kuihakikishia ushindi wa pointi tatu.
Etoile na Mazembe wanajumla ya pointi tatu hadi sasa pamoja na mabingwa wa Zimbabwe, kabu ya Monomotapa, ambao waliichapa klabu hiyo ya Tunisia katika mchezo wa kwanza.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment