TAARIFA KWA VTYOMBO VYA HABARI
TIMU YA TAIFA - TAIFA STARS
Timu ya Taifa – Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa tarehe 12, Agosti, 2009, tarehe ambayo ni maalum kwa michezo ya kimataifa ya kirafiki katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la mpira wa Miguu (FIFA).
Kama ilivyotangazwa awali TFF imekuwa katika jitihada za kutafuta timu ya kucheza na Taifa Stars katika terehe hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa kuiwezesha timu yetu kuwa katika kiwango bora kiuchezaji.
Hivyo TFF inapenda kuujulisha umma kuwa Taifa Stars itacheza na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi). Mchezo huo utafanyika mjini Kigali kuanzia saa 9.30 alasiri.
Taratibu zote za matayarisho ya mchezo huo zinaendelea ambazo ni pamoja na timu kuingia kambini Agosti 3, 2009. Mwalimu wa Taifa Stars, Marcio Maximo atatangaza wachezaji tarehe 30 Julai 2009.
Matarajio ya TFF ni kwamba mchezo huu utasaidia katika kuendelea kuijenga Taifa Stars ambayo mimeendelea kuimarika.
Florian Kaijage
AFISA HABARI
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment