TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
28/07/2009
KIFO CHA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) linasikitika kuuujulisha umma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Ndugu Teofrid Sikazwe amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kifupi.
Taarifa ambazo TFF imezipokea kutoka Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Rukwa RUREFA ni kwamba Ndugu Sikazwe amekutwa na mauti hayo leo jioni majira ya saa kum.
Shemeji wa Marehemu, Philbert Umala ameieleza TFF kuwa ndugu Sikazwe alikimbizwa Katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, mjini Sumbawanga jana (Jumatatu) baada ya kulalamika kubanwa na kifua.
Ndugu Sikazwe ambaye alikuwa pia Katibu wa RUREFA kwa kipindi kirefu, juma lililopita alikuwa jijini Dar es Salaam kuhudhuria Semina iliyoendeshwa na wakufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA) na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika Julai 20, 2009.
Ndugu Sikazwe alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwa mara ya kwanza Desemba 27, 2004 na akachaguliwa tena wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF Desemba 14, 2008.
Ndugu Sikazwe alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF tangu mwaka 2004 kutokana na kuwa na taaluma ya ukocha wa mpira wa miguu na ameongoza misafara kadhaa ya timu za klabu na timu za Taifa katika michezo ya nje ya nchi.
Aliwahi kuwa kocha wa Timu ya Soka ya Ujenzi ya Rukwa na pia mara kadhaa amekuwa kocha wa timu ya Mkoa wa Rukwa katika michuano ya Kombe la Taifa.
TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Taarifa zaidi juu ya ushiriki huo zitatolewa baadaye. TFF inatoa pole kwa wanasoka Mkoani Rukwa na Tanzania kwa ujumla
Mungu aiweke roho ya marehemu Teofrid Sikazwe mahali pema peponi, Amina
Fredrick Mwakalaebela
KATIBU MKUU
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment