Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Simba Msemaji wa Timu hiyo Cliford Ndimbo amesema suala hilo walimalizana siku ya jumamosi katika ofisi za Tff na viongozi wa Mtibwa na tayari wameshatoa kiasi cha shilingi milioni 4 na kiasi kingine kilichobaki watalipa kwa awamu.
Ndimbo amesema Simba imefurahishwa na kitendo cha Mtibwa kuonyesha uungwana kwa kuweza kufikia muafaka na kuwakubalia mchezaji huyo lakini anawaomba busara zilizotumika na wao basi zitumike kwa kumalizana na Coastal Union.
No comments :
Post a Comment