Wekundu wa Msimbazi Simba imewataka wadau na wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda zitakapochuana katika uwanja wa Uhuru Agasti 8 mwaka huu.
Mwenyekiti wa timu hiyo Hassan Dalali amesema siku hiyo itakuwa siku maalum kwa wana Simba kwani itakuwa ikifanyika kila mwaka na kuzaliwa kwa Klabu hiyo.
Dalali ameongeza kuwa mpambano huo utakuwa na lengo la kuwatambulisha wachezaji wapya waliowasajili kwa wanachama wa Simba na Jezi mpya watakazozitumia katika msimu mpya wa Ligi.
Katika mchezo huo Dalali amesema Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano la Tanzania Mh.Samweli Sitta.
Hata hivyo Dalali amesema kutakuwa na mechi ya ufunguzi kati ya timu ya pili ya Simba chini ya umri wa miaka 20 na Afrika Lyon wenye umri kama huo.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment