Vijana wa Mtaa wa msimbazi Simba Sports klabu tayari wamewasili Mkoani Ruvuma kucheza mchezo wake dhidi ya wana lizombe Maji Maji ya Songea ikiwa ni mechi ya ufunguzi ya michuano ya ligi kuu Tanzania Bara msimu huu itakayoanza Agasti 23 mwaka huu.
Afisa habari wa kuajiriwa wa klabu ya Simba Cliford Mario Ndimbo amesema kikosi kimeondoka na wachezaji 23 akiwemo kocha mkuu Patrick Phili,Amri Said kocha msaidizi,meneja Innocent Njovu na mkuu wa msafara, Makamu Mwenyekiti Omary Gumbo.
Ndimbo amesema dhumuni la kwenda mapema Songea ni pamoja na kuzoea uwanja ambao umefanyiwa marekebisho na hali ya hewa ya huko kabla ya kuelekea Mbeya kucheza mchezo mwingine na Tanzania Prison.
Akijibu swali kwa nini wachezaji 5 hawakwenda Songea kujiunga na wenzao Ndimbo amesema wachezaji watatu kati ya hao wana matatizo mbalimbali wakiwemo Ramadhani Chombo,Jabir Aziz ambao ni majeruhi.
Ndimbo ametanabaisha kuwa mchezaji Haruna Moshi Boban ameachwa kwa kuwa amefunga ndoa hivi karibuni lakini kwa wachezaji wawili Olimboka Mwakingwe na George Nyanda wameachwa kwa kosa la utovu wa nidhamu.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment