Yanga iliyo chini ya udhamini mnono wa mfadhili wao, Yusuph Manji wamesajili kikosi cha wachezaji 30 huku wengi wao wakiwa walioipa ubingwa timu hiyo katika msimu uliopita.
Ndani ya kikosi hicho kuna sura mpya za wachezaji wanane ambao sita kati yao ni wachezaji wa kigeni ambao pia wametoka katika timu kongwe Afrika Mashariki.
Wachezaji hao wapya waliomwaga wino Jangwani ni kipa Nelson Kimati aliyetokea Prisons ya Mbega na beki Bakari Mbegu aliliyesajiliwa kutoka katika timu ya Sifa Politan SC inayoshiriki ligi ngazi ya Wilaya ya Temeke.
Yanga iliyochini ya uongozi wa Mwenyekiti Iman Madega ilifanikiwa kunasa saini za wachezaji wa kulipwa Moses Odhiambo kutoka APR ya Rwanda, Kabongo Honore wa DR Kongo, Steven Bengo kutoka SC Villa ya Uganda na Jama Robert Mba kutoka Canon Sportif Yound ya Cameroon.
Pia Yanga walimaliza utata wa wachezaji wake waliowasajili katika dirisha dogo la msimu uliopita lakini wakakosa nafasi ya kuitumikia klabu hiyo John Njoroge na Joseph Shikokoti kutoka Tusker ya Kenya.
Mbali na vifaa hivyo vilivyoongezwa katika kikosi hicho cha Kondic akisaidiwa na Spaso Sokolovics lakini Yanga wamebakisha vifaa vyake muhimu ambavyo vilipeleka shangwe Jangwani kwa misimu miwili iliyopita.
Vifaa hivyo ni Steven Marash, Wisdom Ndhlovu, Athumani Idd 'Chuji', Nurdin Bakari, Nadir Haroub 'Cannavaro', Michael Barasa, Boniface Ambani, Fred Mbuna, Godfrey Boniface, Mrisho Ngassa, Amir Maftah, Obren Curkovic, Shadrack Nsajigwa, Abdi Kassim, Kigi Makasi, Shamte Ali, Vicent Barnabas, Hamis Yusuph na Jerson Tegete.
Wapinzani wa Yanga katika mbio za ubingwa msimu huu wa 2009/10 ni Simba, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Majimaji, Manyema, JKT Ruvu, Prisons, Moro United, Toto African, Azam FC na African Lyon.
Miaka ambayo Yanga imetwaa ubingwa tangu ligi hiyo ianzishwe ni 1965, 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000,2003, 2005, 2006, 2008 na 2009.
Katika usajili wa Simba msimu huu wamefanikiwa kubakisha wachezaji wake wote wa kutumainiwa huku wakiongeza nguvu kwa kusajili wachezaji wapya tisa wakiwemo wa kigeni watatu.
Simba iliwatema wachezaji wake Moses Godwin, Ramadhani Wasso, Nasor Said, Amani Simba na Orji Obinna kutokana na sababu mbalimbali.
Katika kuziba mapengo ya wachezaji waliowaacha na kuongeza nguvu klabu hiyo iliwarudisha wachezaji wake Juma Kaseja aliyesajiliwa Yanga msimu uliopita, Danny Mrwanda aliyekuwa anacheza soka Kuwait.
Mbali na kuwarudisha wachezaji hao walisajili wachezaji wa kigeni, Hilary Echessa wa Kenya, Emmanuel Okwi wa SC Villa ya Uganda na Mganda Joseph Owino kutoka URA ya Rwanda.
Pia waliowaongeza wachezaji Salim Aziz wa Polisi Dodoma,
Amri Kiemba wa Moro United, Uhuru Seleman wa Mtibwa Sugar na Haruna Ramadhani kutoka Toto African.
Vifaa vya Simba vilivyobaki msimu uliopita ambao watakuwa na jukumu la kuwaonesha njia wachezaji wapya ni Haruna Moshi 'Boban', Salumu Kanoni, Kelvin Yondani, Nicco Nyagawa, Adam Kingwande na Musa Hassan 'Mgosi'.
Wengine ni George Nyanda, Ulimboka Mwakingwe, Antony Matangalu, Mohamed Banka, Ramadhani Chombo, Ali Mustapha 'Barthez', Meshack Abel, Jabir Aziz, Deo Munishi, Juma Jabu, Juma Nyoso, Mohamed Kijuso na David Naftar.Wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu wa 2009/10 ni Shaaban Aboma kutoka Toto ya Mwanza, Faustine Lukoo kutoka Miembeni, Pius Kisambale kutoka Moro United, Erick Majaliwa na Monja Liseki kutoka Shaab Hadhramout ya Yemen, Steven Mazanda kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Congo na Said Rashid ambaye ni mchezaji huru.
Wachezaji wa zamani wa Mtibwa waliosajiliwa ni Shaaban Kado, Soud Slim, Omar Ally, Obadia Mungusa, Idrissa Rajab, Geoffrey Magori, Chacha Marwa, Shaaban Nditi, Abdulhalim Humoud, Zuberi Katwila, Zahoro Pazi, Saidi Mkopi, Akilimali Yahaya, Yussuf Mgwao, Uhuru Selemani, David Mwantobe, Omar Matuta, Mwamba Mkumbwa na Soud Abdallah.Kikosi kamili cha African Lyon msimu huu kitaundwa na wachezaji Noel Lucas, Stephano Mkomola, Hamad Waziri, Idrissa Abdallah, Abdallah Mpandachi, Victor Tumbanga, Abdul Mwalami, Yahya Abdallah, Hamis Shengo, Sultan Ali, Mbwana Samata, Mohamed Salehe na Yusuph Soka.
Wengine ni Aziz Issa, Godfrey Komba, Mohamed Samata, Rashid Gumbo, Said Kassimu, Zuber Ubwa, Bakari Omary, Karume Songoro, Castory Mumbala, John Mbugua na Robert Ssentongo.
Wachezaji waliongezwa katika kikosi cha Azam na kufanya kuwa na kikosi cha wachezaji 23 katika msimu huu ni Agrey Morrice kutoka Mafunzo ya Zanzibar na Salum Swedi wa Mtibwa Sugar.
Wachezaji waliotemwa Azam ni Salvatory Ntebe, Shekhan Rashid, James Victor, James Adriano, Malegesi Mwangwa, Paul Nyangwe, Ali Alawi, John Mabula, Kassimu Alimbe Kilungo, Adam Shomari, Yusuph Gogo, Musa Kipao, Zuberi Ubwa, Said Nachikongo na Abdul Hamza.
Pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wachezaji katika kikosi hicho lakini timu hiyo imesheheni wachezaji wengi wenye uzoefu wa michuano mbalimbali.
Wachezaji ambao walikuwa na kikosi hicho katika msimu uliopita ambao tayari watakuwa wameshaelewana vya kutosha ambao watakuwa ni chachu ya kufanya vizuri kwa timu hiyo katika msimu huu ni Crinsine Odula, Danny Wagaluka, Erasto Nyoni, Habibu Muhina, Ibrahimu Mwaipopo, Ibrahimu Shikanda, Jamal Mnyate, John Bocco, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Maridadi Haule, Nsa Job, Osborn Monday, Philip Arando, Said Swed, Salumu Aboubakary, Salumu Machaku, Shabani Kisiga, Yahya Tumbo, Vladimir Niyonkuru na Ben Karama.Kikosi kamili cha maafande wa Prison kwa msimu huu ni Exavery Mapunda, Henry Mwalugala, Laurian Mpalile, Aloyce Adam, Mbega Daffa, Patson Chawinga, Fred Chudu, Ismail Suleiman, John Matei, Shaaban Mtupa, Said Mtupa, Said Mtupa, Misango Magai, Lugano
Mwangama,Sudi Ahadi, Roy Shamba, Ramadhani Katamba, Hashimu Kaongo, David Mwantika,Thomas Baragula na Sylvester Kamtande.JKT Ruvu msimu uliyopita walimaliza ligi wakiwa nafasi ya nne kwa kujivunia pointi 33 na Prisons walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya sita.
JKT Ruvu inaongozwa na Kocha Charles Kilinda ambaye kwa kiasi kikubwa ameifanya timu hiyo kuwa tishio katika ligi ya msimu uliopita na msimu huu imesajili wachezaji 26.
Wachezaji walioachwa ni Enock Mkama, Jumanne Ally, George Osei, Buji Selemani, Munubi Mrisho, Mashaka Maliwa, Gerald Crisant na Lucas Simon.
Wachezaji 26 waliosajiliwa ni Abdallah Ngachimwa, Kessy Mwapande, Rashid Matambo, Shaibu Nayopa, Hassan Kikutwa, Boniface Mwakamele, Sostenes Manyasi, Furaha Tembo, Haruna John, Gryson Kundakila, Amos Mgisa, Bakari Kondo na Abdallah Bunu.
Wengine ni Hussein Bunu, Fullu Masanga, Oscar Gasupina, Shaibu Ally, Charles Thadei, Kisimba Luambano, Simon Shadrack, Mayuki Rajabu, George Minja, Shaaban Dihile, Mwinyi Kazimoto, Damas Makwaya na Stanley Nkomola.Wachezaji waliyosajiliwa na Klabu ya Kagera Suger ni Victor kutoka Uganda na Said Biyunga na Msafiri Juma wote kutoka timu ya Toto African ya Mwanza, Godfrey Taita na Geore Kavira kutoka Villa Squard.
Wengine ni Azoro Ndege kutoka katika timu ya mtaani ya Tumbi ya Kigamboni, Dar es Salaam ambaye uongozi wa timu ya Kagera Sugar ulimwona akiwa anacheza katika Kombe la Taifa katika mkoa wa Temeke na hivyo kuvutiwa naye.
Wengine kuwa ni Sayuni Japhet na Aswele Asukile wakitokea timu ya Yono wilayani Njombe, Iringa ambao walikuwa wakicheza mchuano wa Kombe la Taifa katika timu ya mkoa wa Iringa uliofanyika katika kituo cha Mbeya na walivutiwa na uongozi wa timu hiyo, waliotumwa kwenda mkoani Mbeya kuangalia mchuano hiyo ili kuweza kuwapata wachezaji wapya wachanga wa kuweza kuwasajili.
Makipa Rucheke Musa kutoka timu ya Reli Kigoma na Divito Thomas kutoka katika timu ya Victor nchini Uganda ambayo iko Ligi Kuu nchini humo na ndiye golikipa namba moja wa timu hiyo, ambapo Asukile naye ni golikipa kwa hiyo msimu huu wameamua kusajili makipa watatu wachanga.Kikosi cha Manyema kitakachopambana katika msimu huu ni pamoja na kipa mzoefu Oddo Nombo, Amouh Zulu, Yusuph Silas, Adam Matunga, Mussa Kipao, Patrick Mrope,
Mernard Mgaya, Buju Suleiman, Victory Mwambo, Khalid Sabebe na Boniface Bwilu.
Wengine ni Hamad Mumbi, Mzee Mayala, Ali Suleiman, Shabani Ramadhani, Daudi Maganga, Sandey Juma, Yusuph Nguya, Sixbert Mohamed, Thimos Paul, Musa Omary, Mohamed Khatibu, Julius Mrope, Waziri Khatibu, Benedick Ngassa, Khalfan Omary, Humund Juma na Ali Mohamed.Picha ya timu ya Maji Maji miaka ya Nyuma.
Timu ya Majimaji iliundwa mwaka 1978 mkoani Ruvuma ikitekeleza agizo la Mlale la Siasa ni kilimo ikiambatishwa pamoja na masuala ya kukuza na kuendeleza mkoa katika nyanja za michezo.
Hatua hiyo ilibuniwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa wakati huo, Dkt, Lawrent Mtazama Gama kutokana na mkoa huo kuwa nyuma kisoka, hali ambayo ilikuwa ikisababisha timu kutoka katika mkoa huo kujikuta zikifungwa mabao mengi zaidi ya 10 pale zinapopata nafasi ya kuwakilisha katika mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Je baada ya kufanikiwa kurejea katika ligi kuu TAnzania Bara msimu huu, itaweza kuhimili mikiki kama ilivyohistoria ya klabu hiyo toka Mkoa wa Ruvuma?TOTO African imechukua hadhi ya Pamba ambayo iliufanya mkoa wa Mwanza kutamba katika medani ya soka kwa muda mrefu huko nyuma.
Ikiwa imeanzishwa mwishoni mwa miaka ya 1960, timu hiyo yenye uhusiano wa kidugu na timu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam ina wanachama wasiozidi 50, iliwahi kucheza katika Ligi Kuu mwishoni mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa mwaka 2000 kabla ya kushuka daraja.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro amewataka wananchi wa Mwanza kuwa kitu kimoja katika kuisaidia Toto na kuitaka timu hiyo ijiepushe na kujihusisha na timu moja kubwa kwani hali hiyo inagawa nguvu za wananchi.
Katibu Mkuu wa kwanza kuajiriwa na TFF, Asheri Gasabile, anasema kuwa, ni faraja kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza, kutokana na timu hiyo kubaki Ligi Kuu.
Kocha Choke Abeid anasema uongozi wa Toto African unatakiwa kuboresha dawati la ufundi la timu ya hiyo, baada ya uboreshaji kazi kubwa itakuwa ni kutengeneza timu ya ushindi, kama mwalimu atahakikisha timu inafanya vizuri, ingawa ni kazi ngumu ,
kwa sababu wapenzi wa soka wa Mwanza wangali na hofu na timu yao.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment