Frdrick Mwakalebela ni katibu mkuu wa TFF amesema mchezo wa Simba ni wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya klabu hiyo, Taifa Stars inajukumu la kitaifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda hapo Agosti 12 Mjini Kigali Rwanda.
Mwakalebela amesema katika jukumu hilo uzalendo haunabudi kuwekwa mbele hasa ikizingatiwa timu ya taifa imekuwa ikipata wachezaji toka katika vilabu vya Tanzania ikiwemo Simba.
Mwakalebela amesema anaamini Simba ni binaadamu na wanaelewa umuhimu wa Timu ya taifa pamoja na mchezo huo wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, hivyo anaamini wachezaji hao wataungana na wenzao kambini muda wowote kuanzia sasa.
Aidha Mwakalebela amesema wako tayari kuwaruhusu wachezaji wa Simba kuungana na wenzano wakati wa tamasha la Simba linalotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.
Amewataka wachezaji wa Simba kujiunga na wenzao katika kambi ya timu ya taifa haraka iwezekenavyoo.
No comments :
Post a Comment