Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, December 13, 2012

WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA TANZANIA (JET) WAPEWA MWANGA YALIYOJIRI MKUTANO WA TABIANCHI DOHA




 Ofisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi Stella Vuzo akiwakaribisha waandishi wa chama cha habari za Mazingira Tanzania (JET) na kuwatambulisha wazungumzaji katika mkutano wa taarifa fupi katika kuwapa mwanga kuhusu yatokanayo na taarifa ya mabadiliko ya tabianchi uliofanyika Doha. Katikati ni Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro na kushoto Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.
 
Mkutano huu uliowakutanisha pamoja waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) umeratibiwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo.
Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akielezea kwa ufupi jinsi Umoja wa Mataifa unavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na kufafanua Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumzia yatokanayo mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo swala la Gesi joto ambapo amesema kwa nchi kama Tanzania haichafui mazingira kulinganisha na nchi zinazoendelea zenye viwanda vikubwa pamoja na makubaliano waliyofikikia katika mkutano huo ambayo yatatolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira hivi karibuni.
Mmoja wa waandishi wa habari Bi. Judica Laswai kutoka TBC akieleza namna alivyoweza kupata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa mabadiliko ya tabianchini uliofanyika Doha hivi karibuni kwa kushiriki mashindano ya kuaanda vipindi vya mazingira na mwishowe kushinda safari iliyodhaminiwa ni Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) ambapo amewahimiza wanahabari wenzake kutumia fursa za mitandao ya kijamii.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari za Mazingira (JET) wakiuliza maswali na kutoa maoni kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (hayupo pichani).
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa Mazingira (JET) waliohudhuria mkutano huo.
Ofisa habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma akitoa changamoto kwa waandishi wa habari wa mazingira kuzipa kipaumbele habari za mazingira na kuwataka kuweka usawa katika habari wanazoandika.

No comments :

Post a Comment