Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, December 12, 2012

REDDS MISS TANZANIA 2012 AANZA KAZI RASMI AENDA MKOA WA KAGERA KWA KAZI ZA JAMII.






Redds Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred ameondoka jijini Dar es Salaam, leo tarehe 12 Desemba 2012 kuelekea mkoani Kagera kwa shughuli za Jamii.

Mrembo huyo wa Redds Miss Tanzania, akiwa mkoani Kagera atatembelea Shule maalum ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu, pia atatembelea Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima.

Mrembo Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, [Albinos] atatoa misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na Fimbo maalum za kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya ngozi kwa ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.

Redds Miss Tanzania 2012 pia atatembelea Wilaya ya Misenyi na kutoa misaada kama hiyo katika kituo kimoja kilichopo wilayani humo.

Ziara ya Miss Tanzania 2012 imedhaminiwa na Optima Lodge & Safaris pamoja na Victoria Perch Hotel zote za Mkoani Kagera.

Kabla ya kurejea jijini DSM Redds Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii.

No comments :

Post a Comment