Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, December 26, 2012

FRANCIS CHEKA NA CHIOTCHA CHIMWEMWE WAPIMA UZITO KUZICHAPA LEO SHEIKH AMRI ABEID KUWANIA MKANDA WA IBF



 Mabondia Francis Cheka (kushoto) na Chiokta Chimwemwe wakiwa wameshika mkanda watakaougombea muda mchache ujao jijini Arusha leo, wakati wa utambulisho wao na zoezi la kupima uzito.
 Bondia Francis Cheka akipima uzito

.
 Bondia Chiokta Chimwemwe akipima uzito.

Mabondia Francis Cheka (kushoto) na Chiotcha Chimwemwe, kupigana baada ya kupima uzito na kucheki afya leo asubuhi.
***************************************
Mafahali mawili wanaotegemea kuzichapa tarehe 26, 2012 kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Francis Cheka na Mmalawi Chiotcha Chimwemwe nusura wazichape kavukavu wakati wa upimaji uzito na mkutano wa waandishi wa habari katika hoteli ya nyota 5 yaNaura Springs, jijini Arusha jana tarehe 25 Desemba 2012.



Hii ni mara ya kwanza kwa ngumi za kulipwa kupewa hadhi kubwa kama hiyo ya kuwekwa kwenye hoteli ya nyota tano (5) hapa Tanzania.



Wawili hao walikuwa katika hoteli hiyo ya kifahari ya Naura Springs inayomilikiwa na bwana Felix Mrema anayemiliki mahoteli lukuki katika jiji la Arusha na Moshi ambazo ni Naura Springs Hotel, Impala Hotel, Ngurudito Hotel, Impala Moshi na Livingstone Hotel za Moshi!



Mpambano huo uliopewa jina la “Vurumaini chini ya Mlima Meru”umekuwa ni gumzo katika jiji la Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Manyara pamoja na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda na unaandaliwa na kampuni ya kizalendo ya Green Hills (T) Limited inayomilikiwa na bondia wa zamani wa taifa katika ngumi za ridhaa na kuloipwa George Andrew na familia yake.



Aidha, watalii wengi walioko katika jiji la Arusha wakati huu wa sikukuu ya Xmas wameonyesha nia zao za kuliangalia pambano hili na wengine wameshakata tiketi tayari kuingia katika ujwanja wa Sheik Amri Abeid kuwashughudia mafahali hao wawili wakitoana jasho.



Chiotcha mwana wa Chimwemwe mwanajeshi wa ngazi ya Luteini Usu katika jeshi la Malawi amepania kulibeba juu taifa lake lililoko pembezoni mwa ziwa Nyasa kwa kumwonyesha Francis Cheka kuwa ngumi zinaendana na ushupavu.



Chimwemwe anadai kuwa hakuja Tanzania kutalii kama walivyo watalii wengine bali alikuja kuwakilisha nchi yake aipendayo ya Malawi na kurudi kwao na mshipi wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Alisema kuwa kushinda kwake sio kitu cha kubahatisha ila ni uhakika.



Naye Francis mwana wa Cheka, Mtanzania aliyeipeperusha vyama bendera ya taifa hili katika mapambano mengi bila kuzivunja nyoyo za mashabiki wa ngumi nchini alisema kuwa “Mwache Mmalawi huyo ajifurahishe tu kwani hajui kinachongojea ulingoni”



Cheka aliyejizolea sifa kemkem kati ya mabondia wa kitanzania aliendelea kusema kuwa yeye sio mzungumzaji sana ila ngumi zake ndizo zitakazozungumza siku ya tareeh 26 Desemba, 2012.


“Asifikirie kuwa ngumi ni kupiga makelele tu na ukashinfa” alisema Chelka akimwangalia Chimwemwe wakati alipokuwa anajigamba kwa sifa kemkem!



Mpambano huo wa kukata na shoka unakuja wakati ambako Arusha imekuwa ni jiji na linataka kutumia mapambano mengi ya ngumi ya kimataifa kukuza hadhi ya jiji hilo kama “Geneva ya Afrika” kutokana na mandari yake na mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika katika jiji hili.



Francis Cheka anakutana na Chimwemwe baada ya kuutema mkanda wake wa IBF wakati alipokutana na Karama Nyilawila kugombea mkanda mwingine mbali na IBF hivyo kuupoteza ubingwa wa IBF. Cheka amepania kuuchukua tena mshipi huo na kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ni moto wa kuotea mbali!



Mpambano huo utahudhuriwa na viongozi wengi wakiongozwa na Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo pamoja na wageni wengi wanaofanya kazi kwenye mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita wa Rwanda, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Kati, ILO, UNICEF, WFP na nyingine nyingi.



Aidha watalii wengi wameacha kwenda mbugani siku ya pambano ili washughudie wenyewe ni nani zaidi kati ya Cheka na Chimwemwe.,



Pamabano hilo linaratibiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) chini ya Rais wake Onesmo Ngowi na kupewa baraka zote na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF).


Waamuzi wa pambano ni:


Onesmo Ngowi - Kamishna Mkuu, Roman Chuwa ambaye ndiye Kamishna wa TPBC mkoa wa Arusha –(Kamishna Mkuu Msaidizi), Nemes Kavishe (Refarii), Boniface Wambura – (Jaji), Gallous Ligongo –(Jaji), Mark Hatia –(Jaji).

No comments :

Post a Comment