Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, December 29, 2012

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Wahutubia Jijini Tanga Katika Mkutano wa Hadhara


 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bibi Chiku Galawa akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tanga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na wananchi mbali mbali waliojitokeza kumpokea wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku mbili.
   Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi za ADC zilizorejeshwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho na kujiunga na CUF katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
----
Chama Cha Wananchi CUF kimesema kuwa amani ya kudumu haiwezi kupatikana katika nchi yoyote bila ya kuwepo haki na usawa katika jamii.
Amesema miongoni mwa sera za msingi za chama hicho ni kuwaunganisha wananchi, na kwamba umoja hauwezi kupatikana kwa kuendeleza sera za kibaguzi na kutowatendea haki wananchi.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo wakati akiwahutubia wafuasi wa CUF na wakaazi wa jiji la Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

“Kila mtu ana haki sawa na mwengine kikatiba na kila mtu anastahiki kuheshimiwa haki zake, kwa hivyo nasema tena kuwa popote penye ubaguzi hapawezi kuwa na umoja”, alisisitiza Maalim Seif.
 
Katika Mkutano huo Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amewatanabahisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, na kuacha kushabikia masuala ya kisiasa.
 
“Kikatiba viongozi hawa si wanasiasa bali ni watumishi wa umma, lakini cha kushangaza bado wapo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanajifanya wakereketwa wa vyama fulani na kuwabagua wananchi”, alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.
 
Amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Tanga kwa kuweka kando tofauti za kisiasa na kushirikiana na wananchi katika kusogeza mbele maendeleo ya Mkoa huo.
 
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Tanga bibi Halima Dendegu ambaye alipanda jukwaani kuwasalimia wananchi waliohudhuria mkutano huo, amesema uongozi wa Mkoa huo unashirikiana vizuri na wananchi na wanaishi kwa kupendana na kuheshimiana.
 
Akizungumzia kuhusu uchumi, Katibu Mkuu wa CUF amesema chama hicho kina sera imara za kujenga uchumi wa Tanzania kwa lengo la kuwakomboa Watanzania kuondokana na hali ngumu ya maisha.
Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bado hazijatumika ipasavyo kuweza kuwanufaisha watanzania, na hivyo kuendelea kubakia kuwa nchi maskini.
 
“Ardhi ya Tanzania ina rutba nzuri ambayo takriban inakubali kila aina ya mazao, tuna bahari ambayo nayo ina rasilimali kadhaa wa kadhaa, madini ya kila aina, Tanga kuna bandari na kadhalika, lakini wapi bado rasilimali hizi zinatumika kuwanufaisha watu wachache na makampuni ya kigeni na sisi Watanzani wengi tulio maskini tunabakia kushuhudia mashimo tu”, alifahamisha Katibu Mkuu wa CUF.
 
Amesema iwapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi mwaka 2015, kitahakikisha kuwa wananchi wananufaika moja kwa moja na rasilimali za nchi, na kwamba robo ya mapato yatokanayo na rasilimali hizo yatatumika kulipa madeni ya nje ambayo yameripotiwa kufikia shilingi trilioni ishirini (20).
 
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya chama hicho, Maalim Seif amesema chama bado kiko imara na wala hakitoyumba kutokana na kujengwa na misingi ya imara.
 
“Watakaojaribu kukibomoa watashindwa, CUF hakiwezi kusambaratika hata siku moja kwa kuwa kimejengwa kwa misingi imara na viongozi wake wako imara na madhubuti kabisa”. Alifahamisha.
 
Katika risala yao wafuasi wa CUF Mkoa wa Tanga wameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni upungufu wa dawa pamoja na kuharibika mara kwa mara kwa X-ray katika hospitali ya rufaa ya Bombo Mkoani humo.
 
Nae Naibu Mkurugenzi wa haki za binadamu na mawasiliano ya umma wa CUF bw. Abdul Kambaya amesema rasilimali zilizopo Tanzania zinatosha kuwakomboa wananchi na umaskini, lakini mfumo wa uongozi uliopo bado haujazingatia maslahi ya umma na unalenga kuwanufaisha watu wachache.
“Bandari ya Tanga haifanyi kazi vizuri, reli ya Tanga imekufa, mashamba ya mkonge yamekufa, tujiulize watu wa Tanga kuna nini?” alihoji Kambaya na kudai kuwa limetokana na mfumo uliopo wa uongozi. 
 
Katika Mkutano huo Chama hicho kimepoa kadi ishirini (20) za wafuasi wa Chama Cha ADC walioamua kujiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.

No comments :

Post a Comment