Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 25, 2011

HITMA YA KUWAREHEMU WANAMUZIKI WA 5 STARS YAFANYIKA, SERIKALI KUSAIDIA KUPATIKANA WA KUZIBA PENGO


WANAZUONI WAKIENDELEA NA KISOMO
KUSHOTO NI MMOJA YA WASANII WA KUNDI LA 5 STAR WALIONUSURIKA ALI J PAMOJA NA MWENYEKITI WA SHIWATA KASIM TALIB NA KULIA NI KATIBU MTENDAJI WA BASATA GHONCHE MATERAGO
NAIBU WAZIRI WA HABARI VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO DK.FENELA MUKANGARA KULIA NA KULIA NA KUSHOTO NI MKURUGENZI MSAIDIZI WA UTAMADUNI ANGELA NGOWI.



DAKIKA MOJA KUSIMAMA NA KUOMBEA MAREHEMU

SERIKALI imetoa tamko la kusaidia kupatikana kwa wanamuziki wengine watakaounda kundi la taarabu la Five Stars Modern Taarab baada ya wanamuziki 13 wa kundi hilo kupoteza maisha katika ajali iliyotokea hivi karibuni mkoani Morogoro.

Akizungumza katika dua ya kuwaombea wanamuziki hao jioni ya leo katika hoteli ya Starlight, Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dr Fenela Mukangara alisema vijana wasikate tamaa baada ya vijana hao kupoteza maisha katika ajali hiyo.

Mukangara alisema serikali katika jitihada za kufanikisha azma hiyo watajitahidi kuwasiliana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuzipiga nyimbo za kundi hilo na kusaidia kuuza kazi zilizofanywa na kundi hilo.

Aidha Mukangara alisema Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano kwa muda wote viongozi na familia za marehemu waliokumbwa na msiba huo hapa nchini.

Mukangara alisema watajipanga kuwasaidia vyombo kundi hilo kwa kushirikiana na wadau wa muziki hapa nchini baada ya kundi hilo kupoteza pia vyombo vyake katika ajali hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Henry Clemence alitoa wito kwa wasanii kutunga tungo za kupigia kelele madereva wazembe kwa sababu ajali ndio mojawapo ya matukio yanayomaliza Watanzania wengi.
Clemence ambaye pia ni Mwenyeji wa wanachama wa Taasisi ya Wasanii Tanzania (SHIWATA), Wilayani Mkuranga alisema pengo la wanamuziki hao halitozibika.
Mwenyekiti wa Shiwata, Taalib Cassim alitoa shukrani kwa viongozi wa Serikali kwa kuonyesha kuwajali wasanii ambako Asilimia kubwa ya viongozi wa serikali kupitia Wizara kuhudhuria katika dua ya kuwaombea marehemu walifariki katika ajali hiyo.
Cassim alisema Shiwata inawapenda viongozi wa Serikali kwa kuonyesha kuguswa na tukio hilo ambalo limetingisha Taifa.
Viongozi waliohudhuria katika dua hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Utamaduni, Profesa Hermas Mwansoko, Msaidizi wake Anjela Ngowi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego na wadau mbalimbali wa sanaa.

No comments :

Post a Comment