Kikosi
cha Lindi Soccer Academy (LSA) kilichoshiriki michuano ya Copa Coca
Cola 2013. Wa kwanza kushoto waliosimama, ni Ofisa Habari wa LSA, Salum
Mkandemba, ambaye pia ni Mhariri wa Habari Mseto Blog. Aliyesimama kulia
ni Mkurugenzi wa LSA, Hafidh Karongo na wa kwanza kulia aliyekaa ni
Meneja wa Double M Hotel ya mjini Lindi ambako LSA huweka kambi za
mazoezi.
LINDI, Tanzania
Licha ya kuvuliwa ubinwa, LSA
imeendelea kutawala kikosi cha Copa Coca Cola Kombaini Manispaa ya
Lindi, baada ya kutoa jumla ya vijana 16 katika kombaini hiyo
inayotarajiwa kuingia kambini kesho Jumatatu kujindaa na michuano ya
Copa Coca Cola mkoa wa Lindi itakayofanyika baada ya mfungo wa Ramadhani
TIMU ya Lindi Soccer Academy (LSA), jana imevuliwa ubingwa
wa michuano ya Fifa Copa Coca Cola Manispaa ya Lindi, baada ya kuchapwa mabao
2-0 na Cariacops, katika fainali ya michuano hiyo iliyokuwa ikifanyika kwenye
Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa LSA, Hafidh
Karongo, Cariacops katika mechi hiyo iliibuka kidedea ikibebwa na mabao ya
mapema ya wakali wake George Muta aliyefunga katika dakika ya nane na James
Masheyo dakika ya 30.
Licha ya mabadiliko kadhaa katika jitihada za kujinasua, LSA
ilimaliza pambano hilo
kwa kipigo hicho, kilichohitimisha kipindi chao cha ubingwa waliotwaa mwaka
jana, ingawa imeendelea kutawala kikosi cha Copa Coca Cola Kombaini, Manispaa
ya Lindi.
Karongo aliiambia Tanzania Daima kwa simu kuwa, LSA imetoa
jumla ya vijana 16 katika Kombaini ya Manispaa ya Lindi, inayotarajiwa kuingia kambini
leo kujindaa na michuano ya Copa Coca Cola mkoa wa Lindi itakayofanyika baada
ya Ramadhani.
Aliwataja chipukizi walioteuliwa kuunda Kombaini hiyo kuwa
ni; Harid Selemani, Shaffih Maulid, Ramadhani Amri, Hassan Mkomba, Hassani
Alubuni, Joseph Keneth, Mohammed Omari, Hamis Mahmoud, Midraji Haji na
Ramadhani Bakari.
Wachezaji wengine wa LSA ni pamoja na; Rajabu Msela, Abdul
Shein, Hamdani Sarahani, Hassan Pendeka, Banzalam Hamisi na Yassin Abdallah ‘Iniesta.’
Timu nane zilishiriki Copa Coca Cola Manispaa ya Lindi na kugawanywa katika
makundi mawili.
No comments :
Post a Comment