Kulia
ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake
wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na
kuzalishwa
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu
kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa
kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina
linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya
Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa
kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha
makosa ya kuzini.
akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha
kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa
aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo
alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano
jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti
alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni
kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika
kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia
hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti
pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa
Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa
ulidai kuwa Mshtakiwa ndiye baba
halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na
Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu
alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa
kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la
kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu
Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa
katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani
hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na
Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo
ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa”
Na Mbeya yetu
|
No comments :
Post a Comment