Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ( wa nne kulia)akipata maelezo kutoka
mmoja wa wafanyabiashara wa mihogo Ilala alipofanya ziara rasmi katika
masoko ya Buguruni na Ilala kuangalia utofauti bei za bidhaa kabla na
kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mstahiki Meya
aliwaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa mbalimbali wakati
mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha Waislamu wa mkoa wa Dar kuwa
na mfungo mwema na wao pia kupata Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwani
watawezesha hata wale wenye kipato cha chini kumudu bei bidhaa
zinazotengeneza futari. Mh. Silaa amewatembelea wafanyabiashara katika
masoko kuangalia uwiano wa bei katika masoko hayo.
Mstahiki Meya Jerry
Silaa akiendelea na ziara yake kwenye masoko katika halmashauri yake ya
Ilala akiwa ameambatana maafisa wa mbalimbali wa Manispaa ya Ilala.
--
Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
www.mohammeddewji.com/blog
+255714940992.
No comments :
Post a Comment