Mvutano Bungeni |
Na Bryceson Mathias
HIVI
karibuni Spika Anne Makinda, akijibu maswali ya waandishi kuhusu vurugu
zinazotokea Bungeni, na hasa kuporwa au kugeuzwa kwa hoja za upinzani,
aliibuka na kauli tata akidai vyombo vya habari na waandishi wanahongwa
na wabunge ili waandikwe vizuri.
Ingawa
hakufafanua ni kwa namna gani wabunge wanatoa hongo licha ya kusema
wanatoa kitu kidogo ili waandikwe vizuri, na alikana madai kuwa
anawakandamiza wabunge wa upinzani na kuwabeba wale wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) walio upande wa Serikali.
Makinda
ni miongoni mwa Wabunge, nadhani alitoa kauli hiyo akijisahau kuwa ni
Mbunge, ambapo kwa kuwatuhumu wandishi na vyombo kuhongwa na wabunge
bila kuwataja majina, alikuwa anajijumuisha kwenye Orodha ya wanaotoa
Hongo, aliyoiita kitu kidogo.
Mmoja
wa wabunge wa CCM kanda ya Kusini ambaye hakutaka jina litajwe kutokana
na kukasirishwa na kauli ya Spika kuwaita wananavihonga vyombo vya
habari na wandishi alisema, “Kama wabunge tunatoa hongo, naye ni Mbunge,
basi anatoa pia“.
Mbunge
wa machachari wa (CUF) ambaye mara nyingi huuliza maswali magumu
alisema, Kauli ya Spika anatakiwa aifute mara moja, inaweza ikasababisha
malumbano makali katika Bunge lijalo, ili Spika athibitishe kwa
ushahidi.
Mbunge
wa viti maalum (CCM) kanda ya ziwa alisema, kama Spika hataifuta kauli
yake, amewdhalilisha Wabunge na Bunge, ukizingatia yeye ndiye huongoza
kiti. Kama huwa hawakemei bungeni, akasema nje?, “Ninaangalia uwezekano
wa kumshitaki!”
“Ni
ukweli usiopingika, hata yeye tumekuwa tukimuona akiwakandamiza
wapinzani kama wanavyodai wananchi, hatujawahi kusema anahongwa. Je na
sisi tumtuhumu anahongwa na nani?”. Asipofuta kauli, naandaa hoja
binafsi dhidi yake.
Ingawa
Makinda alijisafisha ati hana upendeleo katika uendeshaji wa vikao vya
Bunge kama anavyoshambuliwa na baadhi ya watu na kwamba lawama
zinazoelekezwa kwake zinatokana na watu kuangalia upande mmoja, Mbunge
huyo alisema, Huwezi kusema huli nyama wakati mchuzi unakunywa!
Aliongeza,
hakuna mtu asiyejua umuhimu wa hoja ya kushuka kwa Elimu na Mustakabali
wake kwa Umma, lakini kuna mambo ambayo kiti katika hoja hiyo kilifanya
sivyo ndivyo, kwa jambo ambalo dhahiri lina maslahi ya umma! Mbona
hatukumtuhumu kama alivyotufanyia?
Makinda
alitoka kuzungumza na Spika wa Korea Kusini, Kang Chang Hee,
alipojinasifu, "Ndiyo najua mnapewa 'kitu kidogo' na hawa wanaoanzisha
vurugu bungeni, lakini kusema Spika anapendelea hili siyo kweli hata
kidogo," alisema Spika.
“Iwapo
ningekuwa na kawaida ya kuwakandamiza wabunge wa upinzani kwa kiasi
kinachosemwa, wengi wa wabunge wa upinzani wasingekuwapo bungeni.
“Mimi
siwapendelei wabunge wa CCM, ningekuwa hivyo hawa wapinzani
wasingekuwapo bungeni,” alisema Makinda muda mfupi baada ya kuzungumza
na ujumbe wa Bunge la Korea Kusini uliomtembelea ofisini kwake.
Hata
hivyo, mbali ya Makinda kusema wakati wa kuendesha vikao vya Bunge
halitakiwi kuwa na itikadi za vyama na kwamba kufanya hivyo kunaweza
kusababisha vurugu, baadhi ya wananchi waliohojiwa walidai, ‘Penye
ukweli uongo hujitenga, Kiti cha Spika akiwemo Makinda kina upendeleo.
Hata
kama Spika alijitetea hivyo, wananchi wamedai wabunge wa upinzani kwa
nyakati tofauti walimtupia lawama za wazi hususani bungeni kwamba
anawapendelea wabunge wa CCM.
Miongoni
mwa mambo yaliyotajwa, amekuwa akilaumiwa kukalia zaidi ya taarifa 10
za ushahidi juu ya kauli za wabunge wa upinzani zilizowasilishwa kwake
kwa muda wote bila kusema lolote. Miongoni mwa ushahidi huo, umo wa
mawaziri kusema uongo bungeni.
Ni
rai yangu kabla ya Makinda kuvinyoshea vyombo habari na wandishi
kidole, ni vema akaangali vidole vitatu vinavyomuuliza. Je wewe!
0715933308
No comments :
Post a Comment