Basi
la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi
wengine hamsini na tatu.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo
lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na
abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
Ajali
hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo
ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya
Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane
maarufu kwa jina la Ntungu.
Alisema
basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake
alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma
kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza
kutoka na kukimbilia kusikojulikana Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu
Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali
hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.
No comments :
Post a Comment