Jumla ya shilingi bilioni 7 zimetengwa na Serikali pamoja na Sekta binafsi kwa ajili ya maandalizi ya wageni watakaokuja Tanzania kabla ya kuanza kwa Michuano ya Kombe la Dunia litakaloanza mwezi Juni hapo mwakani Nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa mkutano wa Wizara ya Miundo Mbinu,Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA Mheshimiwa Shukuru Kawambwa amesema kamati yake inayoundwa na Mawaziri 2 na Manaibu Waziri 3 imeandaa mikakati kabambe kuhakikisha wageni watakuja nchini kwa kuuona na kucheza katika Uwanja wetu Wataifa kabla ya kuanza Michuano hiyo mikubwa ya Kombe la Dunia.
Amesema hatua zilizochukuliwa ni pamoja na mkakati wa kitaifa wa kuhakikisha Tanzania inanufaiki na fainali za kombe la Dunia 2010, na kusema ikiwa ni kuvutia timu shiriki kuja hapa nchini kabla ya kwenda Afrika kusini ambapo tunaamini timu hizo za taifa zitakuja na mashabiki wake ambao watalazimika kulala katika mahoteli yetu lakini wanaweza kupata fursa ya kutembelea sehemu za utalii.
Amesema Kuandaa vivutio ambavyo vitawashawishi watalii ama mashabiki ambao watakuja hapa nchini kabla ya fainali na baada ya fainali za Dunia 2010.
Ameongeza kuwa njia nyingine itakayotumika ni pamoja na kutumia matangazo katika magazeti, tovuti, picha za video na vijarida mbali mbali ambavyo vitakuwa vikielezea vivutio vya utalii wa Tanzania.
Naye Raisi wa Shirikisho la Soka la Tanzania Leodga Chilla Tenga amesema mpaka sasa wanaendelea kuwasiliana na Nchi ambazo zitashiriki Michuano hiyo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika Afrika ijapokuwa kuna ushindani wa hali ya juu katika kufanikisha hilo.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment