TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MICHEZO YA NUSU FAINALI YA KOMBE LA TUKER 2009-12-21
Michuano ya Kombe la Tusker 2009 inaenedelea ambapo sasa michuano hiyo imefikia hatua ya nusu fainali baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi.
Kulingana na ratiba ya michuano hiyo mchezo wa kwanza wa nusu fainali utafanyika Jumatano Desemba 23 ambao utazikutanisha timu za Sofapaka na Tusker zote za Kenya wakati mchezo wa pili utakuwa kati ya Young Africans na Simba SC utakaochezwa Alhamis Desemba 24, 2009.
Mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Sofapaka na Tusker utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru kama ilivyokuwa kwa michezo mingie yote ya Tusker iliyotangulia.
Lakini kutokana na mahitaji ya mchezo wa Yanga na Simba (nusu fainali ya pili) ambao unavutia watu wengi zaidi ikilinganishwa na michezo migine, imeamuliwa kuwa mchezo huu sasa utachezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Uamuzi huu umelenga kuwapa fursa mashabiki, wapenzi na wadau wa mpira kushuhudia pambano hilo bila kubanwa na ufinyu wa uwanja.
Taratibu zote za kupata ruhusa ya kutumia uwanja wa Taifa zimekwishafuatwa na kukamilishwa.
Viingilio na upatikanaji wa tiketi
Viingilio vya mchezo wa nusu faiali ya pili vimegawanywa katika makundi sita
Viti vyote vya rangi ya Kijani na Bluu mzunguko 5,000/=
Viti vya rangi ya Chungwa nyuma ya magoli 8,000/=
Rangi ya chungwa mkabala na jukwaa kuu 10,000/=
Viti Maalum (VIP) C 20,000/=
Viti Maalum (VIP) B 30,000/=
Viti Maalum (VIP) A 40,000/=
Tiketi zimepangwa kuuuzwa kuanzia Jumatano saa 4 asubuhi katika vituo 15 ambavyo vimegwanywa katika wilaya zote tatu za Dar es Salaam (Ilala, Temeke na Kinondoni).
Florian Kaijage
AFISA HABARI - TFF
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment