Timu ya Taifa Kilimanjaro Stars leo imeifunga Burundi goli 1-0 kwenye uwanja wa Mumian nchini Kenya wakati timu hizo zilipokutana kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji Afrika Mashariki na kati, mashindano ambayo mwaka huu yanayofanyika nchini Kenya.
Alikuwa ni mchezaji wa timu ya Taifa Mrisho Ngasa aliyeshindilia goli hilo pekee langoni mwa timu ya Burundi baada ya kupokea pasi nzuri iliyounganishwa na Mussa Hassan Mgosi baada ya kupokea mpira kutoka kwa mchezaji mwingine wa timu hiyo Juma Nyosso.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa sare na kuenda mapumziko zikitoshana nguvu, baada ya mapumziko hayo Kilimanjaro Stars ilipata nguvu zaidi na kujiweka sawa kwa mchezo kitu ambacho kilizaa matunda kwa timu hiyo, Kilimanjaro Stars sasa imefikisha Pointi 4 baada ya kushinda michezo miwili na kufungwa mmoja ambapo ilifungwa na Uganda goli 2, ikaifungaza Zanzibar magoli 1 na leo ikiifunga Burundi goli 1Kalisa Mow wa Rwanda (kushoto) akiwania mpira na Isaias
> Andeberhian wa Eritrea katika mechi ya Kundi B ya kuwania
> Kombe la Chalenji iliyochezwa kwenye Uwanja a Nyayo jana.
> Rwanda ilishinda mabao 2-1.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment