Akizungumza kwa njia ya simu Marwa amesema atampa Matumla kichapo ambacho ajawai kuchapwa tangia ahanze ngumi kwani anajiamini kwa mazoezi aliyofanya nae Matumla amesema kuwa anasubili siku itimie tu kwani yeye ni mtu wa vitendo na si vinginevyo
Pambano hilo limeandaliwa na Ramadhani Uhadi na kuratibiwa na Shumbili Dawa litasimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC).
Akizungumza Dar es Salaam jana mdhamini wa pambano hilo Uhadi alisema maandalizi ya mapambano hayo yamekamilika.
Uhadi alisema mapambano hayo yatatanguliwa na mapambano ya utangulizi kati ya Francis Miyayusho (bingwa wa afrika) na rashidi Ally (bingwa wa Tanzania) (kg54), Chiwa Hussein na Sweet Kalula(kg48), Mbaruku Kheri na Ramadhani Kido (kg 79) na Freddy Sayuni na Omary Ramadhani(kg51).
Aidha mpambano uho uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Uhuru unatarajia kuanza mapema na kutakuwa na ulinzi wa uwakika kwa watu na mali zao.
No comments :
Post a Comment