Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution, Aggrey Marealle (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam kuusu Mashindano ya Chifu Marealle yanayotarajia kuzinduliwa Jumapili ya tarehe 27 desemba 2009, kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa Kampuni hiyo Ibrahimu Kyaruzi.(Picha na Rajabu Mhamila)
Taasisi ya EABL Foundation chini ya kampuni ya East African Breweries ndiyo itakuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kombe la Chifu Marealle yanayotarajiwa kufanyika Mjini Moshi kuanzia tarehe 27 Desemba 2009 mpaka tarehe 2 Januari 2010.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masuala ya Jamii wa East African Breweries, Bw. Ken Kariuki amesema “Sisi EABL tumedhamiria kuboresha maisha ya watu hapa Afrika Mashariki katika njia endelevu”.
Mashindano haya pia yanatumika kutoa elimu kwa vijana kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi na kuwafundisha vijana jinsi ya kuishi maisha bora. "Tunaamini kuwa mashindano haya yataunganisha watu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuweka msingi imara wa vijana na maendeleo ya michezo na kuchangia kutoa elimu kuhusu Ukimwi”, alisema Kariuki.
Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waandaaji wa mashindano hayo Aggrey Marealle alisema zaidi ya timu 14 za soka, timu 7 za netiboli na timu 10 za pool kutoka wilaya za Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha, Hai na Vunjo zote za mkoa wa Kilimanjaro zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu. Mashindano hayo yatafanyika katika kata mbalimbali za manispaa ya Moshi kama vile Pasua, Ikulu KDC, Majengo na viwanja vya George Memorial. Fainali zitafanyika katika uwaja wa MUCCOBS siku kumi baada ya uzinduzi. Timu za soka zitakazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Majengo, Bondeni, Lambo FC, Mawenzi , Kiboriloni, Korongoni, Longuo, Miembeni, Rau, Karanga, Kiyungi, Msaranga, Mji Mpya, Pasua, Soweto, Forest, Njoro, Kilimanjaro, Pasua B, Kaloleni, Langasani na Bafana Bafana
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment