Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka la Tanzania Fredrick Mwakalebela amesema timu ya Ivory Coast itawasili Jumamosi ya wiki hii ikiwa na msafara wa watu hamsini na watafikia hotel ya Kempisk.
Amesema Ivory Coast itacheza michezo miwili mmoja na Taifa Stars Januari 4 na mchezo mwingine itacheza na Timu ya Taifa ya Rwanda Januari 7 kwenye uwanja wa Taifa.
Akitaja viingilio vya mchezo huo Mwakalebela amesema viingilio vitakuwa ni vya aina saba tofauti, ambavyo ni Kijani mzunguko sh 5000, Bluu Mzunguko sh7000, Rangi ya Chungwa nyuma ya magori 10,000.
Rangi ya Chungwa mkabala na jukwaa kuu sh 20,000,
Viti maalum VIP C 30,000
Viti maalum VIP B 40,000
Viti maalum VIP A 50,000
No comments :
Post a Comment