Timu ya Taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars imeichapa Zanzibar Heroes 1-0 na kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Alikuwa ni mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyeipa raha Tanzania Bara baada ya kuunganisha pasi ya kiungo anayecheza soka ya kulipwa nchini Norway, Henry Joseph, na kumtungua kwa shuti kali kipa wa Zanzibar, Ally Muhidin, katika dakika ya 18.
Mchezo wote ulitawaliwa na ubabe baina ya wachezaji kiasi hata Kigi Makassi wa Kilimanjaro na kipa wa Zanzibar, Ally Muhidin, walilimwa kadi nyekundu na mwamuzi Thomas Onyango wa Kenya.
Hii ni mara ya pili katika mwaka huu kwa Bara kuishinda Zenji, kufuatia mchezo wao wa michuano hiyo iliyofanyika mwezi Januari nchini Uganda ambapo Bara ilishinda 2-1.
Eritrea na Zimbabwe zilitoka suluhu 0-0 katika mchezo wa Kundi B wa michuano hiyo uliofanyika jijini Nairobi.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment