Kapteni wa klabu ya Yanga Abdi Kassim Baby kulia akimkabidhi kombe Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Madega (katikati)katibu mkuu Laurence Mwalusako(kulia)baada ya kutwaa uchampion wa michuano ya kombe la Tusker kwa kuifunga klabu ya SOFAPAKA 2-1 katika mchezo wa fainali uliyochezwa uwanja wa Uhuru, jijini dar es Salaam.Wachezaji wa Yanga wakifurahia baada ya kulitwaa kombe la Tusker.Waziri wa habari, utamaduni na michezo George Huruma Mkuchika akimkabidhi kapteni wa klabu ya Yanga kombe la Tusker baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ambapo Yanga iliitandika Sofapaka 2-1.kkutoka kushoto ni golikipa wa Yanga Obren Curcovic, Nadir Haroub "Canavaro", Kigi Makasi na Athumani Iddi "Chuji" wakishangilia baada ya kuvalishwa medali.Kapteni wa klabu ya Sofapaka iliyomaliza ikishika nafasi ya pili akichukua hundi ya Milioni Ishirini.Wachezaji wa Sofapaka wakiwa Hoi baada ya kuzabwa na Yanga 2-1 katika mchezo wa fainali ya kombe la Tusker.Mashabiki wa klabu ya Yanga wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa huku Yanga ikishinda 2-1.Katibu mkuu wa klabu ya Simba Mwina Seif Kaduguda akipokea hundi ya Shilingi milioni kumi ikiwa ni zawadi ya mshindi wa tatu.kama wanaimba vile "Jamani Raha, Jamani Raha eeee Jamani raha, jamani Rahaa eeeeeeeee"IFAHAMU SOFAPAKA KATIKA HISTORIA YAO YA SOKA, KLABU NGENI LAKINI INAYOPATA MAFANIKIO KWA HARAKA, kwanza hii ndiyo maana ya SOFAPAKA.
SOTE (kama) FAMILIA (kwa) PAMOJA KUAFIKIA AZIMIO ndio kirefu cha SOFAPAKA, klabu ya soka iliyoanzishwa kutoka na timu ndogo ya kanisa la M.A.O.S Ministries jijini Nairobi chini ya usimamizi wa Pastor Jimmy Carter Ambajo mwaka 2002.
Klabu hii, ambayo pia ina timu ya wanawake SOFAPAKA QUEENS, imekuwa ikishiriki katika michuano ya kanisa hadi mwaka 2004 wakati mfadhili mkuu ambaye sasa ndiye Rais wao Elly Mboni Kalekwa, mfanyabiashara tajiri mzaliwa wa Congo Kinshasa.
SOFAPAKA, maarufu kama Watoto wa Mungu, iliundwa na timu ya vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu, kabla ya kuanza kununua wachezaji nyota kutoka vilabu vingine vikubwa.
Mwaka huu wamenyakua ubingwa wa Kenya na kuwa timu ya mfano sio kwa Kenya tu bali Afrika Mashariki kwa ujumla, hususan Tanzania kwani ni klabu changa lakini imefanya makubwa na kuna kila dalili itafika mbali.
Pamoja na kuukosa ubingwa wa Tusker 2009, wadau wa soka kwa pamoja tunaipongeza SOFAPAKA kwa kuwa timu ya mfano Afrika Mashariki na Kati.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment