Maonesho hayo yameandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain ikiwa ni mara ya pili kufanyika ambapo awali yalifanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana huku yakishirikisha wanamichezo wa mchezo huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja masoko wa Zain Costantine Magavilla alisema, maonesho hayo yatakuwa ni ya wiki mbili mfululizo ambapo yakiwa yameboreshwa zaidi ili kuweza kutoa burudani ya uhakika kwa watazamaji.
Magavilla alisema, maonesho hayo ni maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu za Krismas na mwaka mpya ambapo wakazi wa Arusha watafurahia shamrashamra hizo.
Alisema sambamba na maonesho hayo pia watachezesha droo kutoka kwenye majina na kadi za biashara watakazo kuwa wakiacha wateja pale wanapoingia kushuhudia maonyesho hayo.
Alisema washindi katika droo hiyo watajipatia vifurushi vya Zain vya huduma ya intaneti, kila siku hadi mwisho wa maonesho hayo.
No comments :
Post a Comment