Nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi ametajwa na shirikisho la kandanda Duniani Fifa kuwa mchezaji bora wa Mwaka 2009 wa timu ya taifa ya Argentina.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye ameisaidia klabu ya Barca kutwaa uchampion wa mashindano ya klabu ya Dunia siku ya Jumamosi – na kujikusanyia jumla ya makombe sita mwka huu, lakini pia Messi alitwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Ulaya maarufu kwa jina la Ballon d'Or.
Ni mwaka wa mgumu na wamafanikio kwangu kumaliza nikiwa mchezji Bora, amesema Messi.
Messi amemmwaga mwanamichezo bora wa mwaka jana Cristiano Ronaldo, pamoja na wachezaji wengine nyota akiwemo Xavi Alonso, Kaka na Andres Iniesta.
Katika kura zilizopigwa na Makpteni, makocha wa soka la wanawake wa timu za taifa, Messi alijikusanyia jumla ya kura 1,073, Ronaldo 352, Xavi 196, Kaka 190 na Iniesta 134.
Messi anakuwa mchezaji wa kwanza toka Argentine kushinda tuzo hiyo, ambayo ilianzishwa mwaka 1991.
Nyota huyo ameiwezesha Barca kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, La Liga na kombe la Hispania msimu uliyopita, utakumbuka msikilizaji alifunga goli la pili katika mchezo ambao walishinda 2-0 dhidi ya Manchester United mjini Rome mwezi May.
Msimu huu klabu hiyo toka Catalan imefakiwa kutwaa ubingwa wa Spanish Super Cup, European Super Cup na Club World Cup katika kuthibitisha kwmaba wanahitaji heshima, wakiifunga klabu ya Estudiantes ya Argentina huko Abu Dhabi na kumaliza wakiwa Miamba wa soka mwaka huu.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Messi alimbwaga Ronaldo katika tuzo ya mwanasoka bora wa Ulaya jumla ya pointi 473 kwa pointi 233 – na sasa amefanikiwa kuchukuamikoba ya Ronaldo kwa kushinda tuzo ya Fifa ya mwanasoka bora wa Dunia.
Hata hivyo, Messi akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo amesema, yeye si mfalme wa soka wa Dunia kwa sasa, siyo nambari moja na wala haamini mambo hayo.
Amesema yeye ni mchezaji wa kawaida kama walivyo wengine lakini anatamani kuwa bora zaidi kila siku na kucheza timu kubwa, amedai umekuwa ni mwaka mzuri kwa Barca na kwake na kumshukuru kila mmoja ambaye amepelekea yeye kupata mafanikio.
Katika hatua nyingine, nyota wa England John Terry na Steven Gerrard wametajwa katika kikosi cha wachezaji 12 wa FIFA ama unaweza kuita timu ya mwaka ya FIFA.
Mchezaji mwingine wa ligi kuu ya England Patrice Evra, Nemanja Vidic na Fernando Torres nao wamechaguliwa pamoja na nyota wa zamani wa Manchester United, Ronaldo.
Golikipa wa Real Madrid, Iker Casillas, wachezaji wa Barca ni Dani Alves, Xavi, Iniesta na Messi wanakamilisha idadi ya wachezaji 12.
Cristiano Ronaldo hakutoka kappa kwa alitajwa kuchukua Fifa Puskas Award ama unaweza sema ndiye mchezaji aliyefunga goli bora la mwaka kwa shuri kali la umbali yadi 40 wakati akiichezea Manchester United katika mchezo dhidi ya FC Porto ikiwa ni katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabigwa barani Ulaya mwezi April.
Mbrazili, Marta ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka katika soka la wanawake na kuweka rekodi ya kutwa tuzo hiyo miaka minne mfululizo, akimbwaga mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa ya wanawake wa England, mshambuliaji Kelly Smith.
Kelly Smith mwenye umri wa miaka 31 ambaye anaicheza soka katika klabu ya Marekani, alianza kucheza soka nchini England na kuiwezesha kufika nusu fainali ya michuano ya
FIFPro team of the year: Casillas; Dani Alves, Evra, Terry, Vidic; Xavi, Iniesta, Gerrard; Ronaldo, Messi, Torres.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment