Kipa wa JKT Ruvu Juma Dihile, akiwa katika harakati za kuokoa mashambulizi langoni mwake, mbele ya Jerry Santo wa Simba. Na Sufianimafoto Reporter, jijini
Timu ya Simba ya Dar es Salaam, leo jioni imeshindwa kuonyesha cheche zake kwa JKT Ruvu ili kufuta machungu waliyoyapata mwishoni mwa wiki iliyopita ilipofungwa mabao 3-2 na TP Mazembe na kulazimisha sare ya 1-1
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, JKT Ruvu ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 27, kupitia kwa mchezaji wake Hussein Bunu, ambalo lilidumu hadi kilipomalizika kipindi cha kwanza, hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Simba ilikuwa nyuma kwa bao 1-0.
Simba iliweza kupata penati katika dakika ya 85 baada beki wa JKT kuunawa mpira akiwa eneo la hatari. Penati hiyo ilipigwa na Emmanuel Okwi na kuandika bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kw sare ya 1-1.
Baada ya penati hiyo kipa wa JKT Juma Dihile, alipewa kadi nyekundu na kuleta utata kwani tayari JKT ilishamaliza sabu zake na kuwalazimu kumteuwa mchezaji wa ndani kuokoa jahazi kwa kukaa golini kuokoa jahazi.
Na baada ya dakakia kadhaa baadaye mchezaji mwingine wa JKT Ruvu alipewa kadi nyekundu na kubaki wachezaji tisa ndani ya uwanja hadi unamalizika mchezo huo.Mwamuzi wa mchezo huo na wasaidizi wake, wakitolewa uwanjani hapo chini ya usimamizi wa Askari.
No comments :
Post a Comment