Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” Jumamosi tarehe 30-04-2011 inataraji kutumia onyesho lake katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, kuwasugulisha kisigino washiriki wa shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.
Sugua Kisigino ni mtindo unaotumiwa na Twanga Pepeta na ni moja ya staili zitakazotumika kwenye shindano hilo, hivyo washiriki watatumia fursa hiyo ili kufahamu jinsi ya kucheza staili hiyo.
Washiriki watatumia onyesho hilo ili kusalimu mashabiki wa Mango Garden ukumbi ambao una historia ndefu na Twanga Pepeta.
Onyesho rasmi la utambulisho wa Vimwana wa Twanga Pepeta 2011 unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 06-05-2011 ndani ya Club ya Sun Cirro iliyoko Sinza na Fainali itakuwa Ijumaa tarehe 03-06-2011.
Burudani ya Utambulisho wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 itatolewa na Wakali wa Dansi Tanzania, African Stars Band “Twanga Pepeta” na Msanii Abbas Kinzasa maarufu kama 20 percent au asilimia ishirini, pamoja na shoo kali ya Nyonga teketeke ya Vimwana wa Twanga Pepeta.
MAIMARTHA JESSE
MRATIBU WA SHINDANO.

No comments :
Post a Comment