Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imekamilisha mashindano ya kuchoma nyama katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo yamefanyika kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa wananchi wa mikoa hiyo
Akizungumzia fainali hiyo ya aina yake, Meneja wa Bia ya Safari lager Fimbo Butallah alisema fainali za mwaka huu katika mikoa hiyo zimekuwa za kufana na kwa mafanikio makubwa jambo ambalo limepelekea kufanikiwa kwa malengo ya safari larger katika kuasisi na kuendesha mashindano hayo
Alisema lengo kuu la mashindano hayo ni kuwezesha maboresho katika maeneo ya baa na pia kusaidia kukuongeza ujuzi kwa wachoma nyama ili kuwezesha wanywaji wa beer za safari kupata fursa ya kula nyama choma bomba huku wakishushia na safari lager baridi
Katika kufanikisha haya beer ya safari iliweza kuwatafuta majaji mahiri waliobobea katika maswala ya utayarishaji,uchuaji wa nyama na uchomaji ambao wamepata utaalam wao katika nchi mbalimbali zilizobobea kwenye taaluma hiyo
Kwa upande wao wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro katika hutuba zao zilisomwa kwa niaba yao na wawakilishi wao walisema serikali itahakikisha inawasaidia na kuendeleza juhudi za bia ya safari katika kuhakikisha wanywaji wa beer wanapata nafasi ya kula nyama choma bomba huku wakiwataka baa zote zilizofanikiwa kuingia kwenye hatua ya tano bora kwa mioa hiyo kuendeleza ubora wa uchomaji wa nyama ili kuweza kuhakikisha wanabakia katika nafasi za ubora walio nao kwa hivi sasa
Mahindano ya hayo mkoani Arusha yalishirikisha baa za Songambele ambao ni washindi wa kwanza, sakina baaa washindi wa pili,Angels pub washindi wa tatu, Arusha Night Park washindi wan ne na washindi wa tano ni QX Pub ambapo fainali zake zilifanyika katika viwanja vya AICC Club huku mkuu wa mkoa hua akiwakilishwa na meya wa Jiji hilo Bwana Lyimo
Mkoani Kilimanjaro baa zilizoingia hatua ya tano bora ni Makanyaga bar ambao ni washindi wa kwanza, East Africa bar washindi wa pili, Mkulima Bar washindi wa tatu,Green Garden bar washindi wan nne na White star washindi wa tano ambapo fainali zilifanyika katika Hotel ya Hugos iliyopo mjini Moshi
Aidha fainali hizo zilipamwa na burudani toka katika bendi za Ndanda Cosovo na Family bend ambazo ziliweza kutoa burudani murua kwa maelfu ya wapenzi wa beer na nyama choma waliofurika katika fainali hizo ambapo fainali mkoani Arusha ilikuwa jumamosi ya 26/03/2011 na mjini moshi ni jumapili ya 27/03/2011
No comments :
Post a Comment