Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
kinatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Mtenda SunSet
uliopo Soweto Jijini Mbeya. Mratibu wa Shindano hilo Fredy Herbet,
amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda kukaa
kambini tangu Juni 25, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali
wanatarajia kuivunja Juni 29, Mwaka huu baada ya Msindi kupatikana.
Ameongeza kuwa Shindano hilo limeandaliwa na Lake Victoria Arts &
Culture Promotion chini ya Udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha
REDDS, SBC kupitia Mountain Dew, Man Company, My Choice Botique, Ebony
Fm na Bomba Fm radio. Amesema kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na
burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia ya Jijini Dar Es Salaam na
kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 10,000/= kwa watu wa kawaida
na 25,000/= kwa VIP. Amewataja washiriki wanaong’ang’ania kuibuka
kidedea kwa kuiwakilisha Kanda katika shindano la kumpata Miss Tanzania
Mikoa wanakotoka kwenye mabano na namba aliyoshinda Mkoani kwake kuwa
ni pamoja na Lina J. Allan (Rukwa 1), Aneth B Mapugilo(Mbeya 2), Jesca
Mikambi(Katavi 2), Nuru Baraka ( Katavi 1) na Neema Mality (Iringa 1).
Wengine ni Lucy George (Iringa 3), Nuriath Suleiman (Njombe 1), Evamary
Gamba( Rukwa 2) Lilian Samson (Iringa 2), Naba Magambo (Mbeya 4),
Jacklin J Luvanda (Mbeya 1) na Winfrida Felix Miss Njombe namba 2. Kwa
Upande wake Mwalimu wa Walimbwende hao Naomi Jones ambaye ndiye
anayeshikilia taji hilo amesema kambi iko vizuri na washiriki wote
wanafuata maelekezo vizuri hivyo Majaji wawe makini kumtafuta Msindi
kutokana na wote kuwa na sifa zinazofanana.
Na:Mbeya yetu
No comments :
Post a Comment