Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya
Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo amesema
kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa kifedha ILO iliweza
kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi mbalimbali wenye vipato
vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia Makongamano, Semina na
Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo la kazi Duniani.
Ameongeza kuwa “tuliwasaidia kuwaunganisha
na vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji midogo midogo
ya kufungua biashara ndogo ndogo katika harakati za kuwafanya
wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya Ngono isiyokuwa Salama.
Bw. Musindo amesisitiza Umuhimu wa TACAIDS
kuandaa makongamano kama haya ili kuwawezesha wasichana na wavulana
wadogo kupata ufahamu uelewa na mafunzo ya uzazi wa Afya na jinsi ya
kuelewa mabadiliko yao ya kimaumbile.
“Ni matumaini yangu mwingiliano huu wa
Utamaduni wa kupambana na Ukimwi, Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi
umefanyika vizuri, hasa katika kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira
magumu itasaidia kuongeza kasi ya kupunguza maambukizi mapya kama
ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi
mapya yamepungua kwa Asilimia 20”. Amesema.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii,
Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa
Wizara hiyo amesema mikakati ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi inaweza
kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake,
Wasichana na Wavulana wadogo.
Amesema Jamii lazima itambue kuwa juhudi
zaidi zinahitajika ili nchini yetu iweze kufikia malengo ya 0.3 yaani
Tanzania ambayo haina maambukizi mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu ya
vifo, vile vile pasipo unyanyapaa wala ukatili kwa mtu yeyote anayeishi
na Virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na washiriki amesema Takwimu
zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya hatari ya kuambukizwa zaidi
kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia Sita ya Wanawake nchini
huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini nzima.
Dr. Mrisho alisisitiza umuhimu wa kumwezesha
mwanamke kiuchumi kama ndio moja ya suluhisho la kumfanya kutokuwa
tegemezi katika jamii.
“Amesema takwimu zinazonyesha katika nchi
nyingi za Kiafrika umaskini unachagia sana kuenea kwa Ukimwi maana
Wanaume wengi hutumia umasikini wa Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa
fedha na kufanya nao Ngono isiyosalama”.
Dr. Fatma Mrisho amepongeza juhudi za ILO na
kuwataka mashirika mengine na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi kuiga
juhudi zilizofanywa na ILO za kuandaa makongamano ya kiuchumi ili
kumwezesha Mwanamke na wavulana wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao
katika mapambo ya VVU na Ukimwi nchini.
No comments :
Post a Comment